Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Emmanuel Lekishon Shangai
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ngorongoro
Primary Question
MHE. EMMANUEL L. SHANGAI aliuliza:- Je, lini Serikali itatenga fedha za ujenzi wa Daraja la Mto Juhe, Kata ya Samunge?
Supplementary Question 1
MHE. EMMANUEL L. SHANGAI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa majibu ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza swali la kwanza; kwa sasa hivi mvua zinaendelea kunyesha na wananchi wanashindwa kupeleka mazao kwenye masoko yao na wanafunzi wanashindwa kwenda shuleni. Kwa nini Serikali isichukulie ujenzi wa daraja hili au usanifu wake kwa haraka kwa sababu wananchi wanashindwa kufanya shughuli zao?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; kuna daraja la aina hiyo hiyo la Mto Piyaya, Serikali ina mpango gani kwa ajili ya kufanya usanifu pamoja na kujenga? Ahsante.
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge amekuwa akifanya ufuatiliaji wa hali ya juu kuhusiana na miundombinu ya daraja hili la Mto Juhe katika Kata ya Semunge. Pia amekuwa akifanya ufuatiliaji wa kuhakikisha kwamba, miundombinu ya barabara katika jimbo lake inaimarika. Amekuwa akifuatilia ahadi ya Makamu wa Rais ya kilomita 12 zote hizi amekuwa akihakikisha kwamba anataka kuona kwamba wananchi wake wanaweza kupatiwa suluhu na miundombinu hii inaweza kuimarishwa katika jimbo lake.
Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kama nilivyojibu kwenye majibu ya msingi katika Mwaka wa Fedha 2025/2026 tutaanza na usanifu wa Daraja hili la Mto Juhe ili hatimaye tuweze kutenga bajeti na kuijenga daraja hili ili liweze kuwanufaisha wananchi wako.
Mheshimiwa Spika, hali kadhalika katika Daraja hili Mto Piyaya na lenyewe tutalifanyia usanifu ili tuweze kufahamu gharama ya ujenzi wa daraja hilo, tuweze kulijenga kwa ajili ya manufaa mapana ya wananchi wako na tutaendelea kuhakikisha kwamba tunachukua hatua za dharura kwenye mazingira ambayo mawasiliano yamekatika ili wananchi wasikwame katika shughuli zao za uchumi na wasikwame katika kupata huduma za msingi za kijamii.
Name
Abubakar Damian Asenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilombero
Primary Question
MHE. EMMANUEL L. SHANGAI aliuliza:- Je, lini Serikali itatenga fedha za ujenzi wa Daraja la Mto Juhe, Kata ya Samunge?
Supplementary Question 2
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Spika, tunaishukuru TARURA kwa kutupatia machuma ya kivuko cha Kidatu Kati na Kidatu A inayohusisha na barabara ya Chikago ambayo Mkandarasi ameondoka kwa muda mrefu. Je, ni lini Serikali itamsimamia mkandarasi yule kurudi ili kukamilisha ile barabara ya Chikago na Kivuko?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu mkubwa sana wa miundombinu ya barabara hizi za wilaya zinazosimamiwa na TARURA na Serikali imekuwa ikitenga bajeti kila mwaka kuhakikisha kwamba, inawekeza zaidi katika kuimarisha miundombinu hii.
Mheshimiwa Spika, katika utengaji wa fedha hizo, imehakikisha inasimamia utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu hii ya barabara za TARURA kwa umakini mkubwa sana.
Mheshimiwa Spika, ninaomba nitumie nafasi hii kuendelea kumhakikishia Mheshimiwa Asenga Abubakari kwamba, Serikali itaendelea kufuatilia na kuhakikisha, ujenzi wa miundombinu ya barabara hii aliyoitaja na eneo hili la daraja alilolitaja unakamilika ndani ya muda wa kimkakati.
Name
Abdallah Jafari Chaurembo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbagala
Primary Question
MHE. EMMANUEL L. SHANGAI aliuliza:- Je, lini Serikali itatenga fedha za ujenzi wa Daraja la Mto Juhe, Kata ya Samunge?
Supplementary Question 3
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Spika, ni lini ujenzi wa Daraja la Mto Majisaku utaanza ambao mkataba wake ulishasainiwa?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, naomba nimtaarifu Mheshimiwa Abdallah Chaurembo kwamba, daraja hilo alilolitaja ujenzi wake utaanza mara moja kwa maana ya mchakato wote wa kumpata mkandarasi umekamilika na sasa punde wataona kabisa kazi hii ya ujenzi wa daraja hili muhimu kabisa kwa wananchi wake unaanza.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved