Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Margaret Simwanza Sitta
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Urambo
Primary Question
MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kusafisha na kuweka uzio Uwanja wa Ndege Urambo kwa kuwa ni muhimu kwa Biashara ya Tumbaku na ni Uwanja wa dharura?
Supplementary Question 1
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ili niulize maswali. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri kuhusu swali nililouliza bado narudi kwa Serikali kuiuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kutokana na kwamba Uwanja wa Ndege wa Urambo upo katikati ya Mji na umuhimu wake kwa ajili ya dharura ya ndege kutua pale na kadhalika, kweli Serikali yetu ilivyo makini inaweza kushindwa kuweka uzio ili kuutunza uwanja wenyewe lakini pia kwa ajili ya usalama wa wananchi? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili; je, kwa jinsi ilivyo makini Wizara ya Uchukuzi, kweli imeshindwa kuweka watu wa kufanya usafi ili na sisi mji wetu upendeze? (Makofi)
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, kupitia Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Mbarawa nimpongeze sana Mheshimiwa Mama yetu Sitta kwa ufuatiliaji mkubwa anaoufanya wa shughuli za maendeleo katika eneo lake na pia, kwa kutambua kwamba Serikali hii ni makini. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Mama yetu Sitta kwamba Serikali kama nilivyosema ni makini na inao mpango huo, lakini atupe muda tu kama nilivyokuwa nimeeleza kwenye jibu la msingi.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na jambo la pili la usafi. Ninamwelekeza Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege kupitia timu yake waende kwenye eneo hilo na waendeleze programu ya kufanya usafi ili uwanja huo uweze kuwa msafi. (Makofi)
Name
Hassan Seleman Mtenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtwara Mjini
Primary Question
MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kusafisha na kuweka uzio Uwanja wa Ndege Urambo kwa kuwa ni muhimu kwa Biashara ya Tumbaku na ni Uwanja wa dharura?
Supplementary Question 2
MHE. HASSAN S. MTENGA: Mheshimiwa Spika, Mtwara ni Mji ambao unakua na tukilinganisha tupo mpakani mwa Msumbiji na Comoro. Ni lini Serikali itatujengea meli kwa jili ya kuendelea na suala letu la kibiashara Mtwara - Comoro na Mtwara – Mozambique. Ahsante sana. (Makofi)
SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, sijamsikia vizuri, anazungumzia meli siyo?
MHE. HASSAN S. MTENGA: Mheshimiwa Spika, ninazungumzia meli.
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, okay. Kwanza nimshukuru Mheshimiwa Mtenga anavyofuatilia maendeleo katika Jimbo lake. Serikali inajenga meli mbalimbali katika Maziwa Makuu na hivi mwezi uliopita imekamilisha mpango wa kumkabidhi msanifu. Tumeshaanza usanifu wa kina na upembuzi yakinifu kwenye Bahari ya Hindi ili tuanze kujenga meli ambayo itakuwa inafanya shughuli zake kwenye Mwambao wa Bahari Hindi ikiwemo Mtwara, Lindi, Tanga, Zanzibar na maeneo mengine yote ambayo yanapakana na Bahari hiyo.
Name
Priscus Jacob Tarimo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Mjini
Primary Question
MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kusafisha na kuweka uzio Uwanja wa Ndege Urambo kwa kuwa ni muhimu kwa Biashara ya Tumbaku na ni Uwanja wa dharura?
Supplementary Question 3
MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana. Ni lini Serikali itakamilisha ukarabati wa Uwanja wa Ndege wa Moshi?
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nimshukuru Mheshimiwa Tarimo kwa ufatiliaji na yeye ni shahidi tulikuwa wote kutembelea uwanja huo hivi majuzi kwenye eneo hilo. Tunaendelea na taratibu mbalimbali za ndani ili kuweza kumlipa Mkandarasi aweze kuendelea na hatimaye akamilishe ujenzi wa uwanja huo wa Moshi ambao ni muhimu sana kwa maslahi ya nchi yetu. (Makofi)
Name
Jesca Jonathani Msambatavangu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Iringa Mjini
Primary Question
MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kusafisha na kuweka uzio Uwanja wa Ndege Urambo kwa kuwa ni muhimu kwa Biashara ya Tumbaku na ni Uwanja wa dharura?
Supplementary Question 4
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, Uwanja wa Ndege wa Iringa umewekewa uzio na una usalama wa kutosha, lakini ndani ya ule uwanja kuna Shule ya Msingi inayotumika. Je, watatusaidiaje ili kuondoa watoto mle ndani kwa sababu ndege kubwa zimeanza kushuka pale?
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge wa Iringa Mjini kwa ufuatiliaji wake makini wa Uwanja wetu wa Iringa. Ninataka nimhakikishie kwamba taratibu mbalimbali zinaendelea kufanyika ili kuhakikisha jambo hilo linafanyika kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi yetu.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved