Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Cecilia Daniel Paresso
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO K.n.y. MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Je, kwa nini Mabwawa ya Samaki yaliyopo Kata ya Kalemawe – Same yasikabidhiwe kwa wananchi wa Kata hiyo?
Supplementary Question 1
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, ninaomba niulize maswali madogo mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa, Serikali imekiri kwamba mabwawa hayo yapo chini ya halmashauri na tunaelewa uwezo wa halmashauri zetu kimapato wakati mwingine ni madogo na hayakidhi mahitaji. Je, Serikali haioni umuhimu sasa kupitia Miradi ya BBT kuziwezesha Kata husika ili ziweze kuendeleza mabwawa haya? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili; ukiacha kwamba samaki ni biashara lakini ni chakula muhimu kwa afya na wananchi wengi pia wanaona kwamba, kufuga samaki kupitia mabwawa madogo madogo ni gharama kubwa, lakini pia wanashindwa kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao. Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba, inatoa elimu na mitaji kwa wale wananchi ambao wana utayari ili na wao waweze kufuga samaki hao kuliko kutegemea tu samaki walioko katika mabwawa na maziwa makubwa? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Moja, ni kwamba Wizara tumeshakubali kwamba tutashirikiana na halmashauri ili tuone namna bora ambapo yale mabwawa yatakabidhiwa kwa wananchi. Unapotaka kukabidhi mabwawa yale kwa wananchi maana yake ni lazima Wizara tuwawezeshe wananchi wale ili waweze kuwa na uwezo wa kuyaendesha yale mabwawa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hata katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuna Mradi wa BBT Life kwa maana ya livestock and fisheries ambao unatekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini. Kwa hiyo, jambo lako tumelipokea na tutaliweka katika huo mpango. Ahsante.
Mheshimiwa Spika, kuhusu mkakati ni kwamba hilo lipo la kuendelea kuelimisha wananchi ili waweze kuchimba mabwawa na kuwapatia mitaji, ndiyo maana imehimizwa sasa hivi watu wengi waweze kufanya ufugaji wa samaki kupitia haya mabwawa. Kwa hiyo, hilo jambo lipo na linafanyiwa kazi. Kwa hiyo, kikubwa sisi tutaaongeza msukumo tu kuwafikia wananchi. Ahsante. (Makofi)
Name
Nashon William Bidyanguze
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kigoma Kusini
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO K.n.y. MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Je, kwa nini Mabwawa ya Samaki yaliyopo Kata ya Kalemawe – Same yasikabidhiwe kwa wananchi wa Kata hiyo?
Supplementary Question 2
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE: Mheshimiwa Spika, ninaomba kuiuliza Serikali ni lini itapeleka vifaranga kwa ajili ya wale ambao wamekwishapewa vizimba katika Ziwa Tanganyika? Ahsante. (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, ni kweli anachokisema Mheshimiwa Mbunge Bidyanguze. Moja kati ya mkakati wa Serikali ni kuhakikisha wananchi wengi hususan katika maeneo ambayo wana maziwa kwa maana ya Lake Victoria, Tanganyika na Nyasa wanaingia katika ufugaji wa samaki kupitia vizimba.
Mheshimiwa Spika, moja ya wajibu wetu ni kuendelea kuzalisha vifaranga vingi kuwawezesha wavuvi ili waweze kufuga kisasa, hivyo jambo hili lipo na nikitoka hapa nitazungumza na Katibu Mkuu nione wamefikia wapi katika uzalishaji wa vifaranga ambavyo vitawawezesha kuwafikia wavuvi wote. Ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ilemela
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO K.n.y. MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Je, kwa nini Mabwawa ya Samaki yaliyopo Kata ya Kalemawe – Same yasikabidhiwe kwa wananchi wa Kata hiyo?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa ufugaji wa samaki kwa njia ya mabwawa pamoja na vizimba unaonekana una tija kubwa. Je, ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba vijana wanojitokeza kuomba mikopo kwa ajili ya ufugaji wa vizimba wanapata mikopo hiyo? Ahsante sana. (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Ni kweli anachokisema Mheshimiwa Mbunge moja ya mkakati wa Serikali ni kuingia katika ufugaji wa samaki kupitia vizimba. Sasa hivi msisitizo umekuwa mkubwa sana. Moja ya mkakati mkubwa katika kuwawezesha hawa watu ni kwamba, kupitia Rais alitoa maelekezo kwa benki zote nchini katika lile dirisha la kilimo ambalo linalisha kilimo, mifugo na uvuvi kupunguza riba kwa kiwango kikubwa. Vilevile, tuna fedha ambazo zipo katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa ajili ya kuwawezesha wafugaji. Kwa hiyo, vijana wajitokeze watimize hayo masharti na wapatiwe mikopo kwa ajili ya huo ufugaji wa samaki kupitia vizimba. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved