Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Oliver Daniel Semuguruka
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kuanza ujenzi wa Kituo cha Forodha Kijiji Mukikoro Kata ya Mugoma – Ngara?
Supplementary Question 1
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Ninalo swali moja la nyongeza. Mchakato wa ujenzi wa kituo hiki cha forodha katika Kijiji cha Mkikomero Kata ya Mugoma, Wilaya ya Ngara ulianza una miaka zaidi ya miwili sasa tangu uanze. Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa kituo hicho ili kuweka hata makontena tusiendelee kupoteza mapato katika Serikali yetu?
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, kwanza ninaomba nimpongeze sana Mheshimiwa Oliver kwa kazi kubwa sana na juhudi anayofanya katika ufuatiliaji wa ujenzi wa kituo hicho. Ninaomba nimhakikishie kwamba juhudi yake imezaa matunda mazuri na hivi karibuni kwa sababu fedha imekwishatengwa kituo hicho kitaanza kujengwa mara tu baada ya mwaka wa fedha unaokuja.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved