Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Rose Vicent Busiga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:- Je, lini Serikali itawalipa mafao yao mashujaa wa Vita vya Kagera na Uganda?
Supplementary Question 1
MHE. ROSE V. BUSIGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; ni lini maboresho ya Sheria ya Pensheni na Kiinua Mgongo ya Mwaka 1966 yataletwa Bungeni?
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; kwa kuwa mashujaa hawa wengi wao wana hali ngumu ya kimaisha, ni lini Serikali itaweza kuwapa msaada wa dharura ili waweze kusaidika?
Name
Dr. Stergomena Lawrence Tax
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nominated
Answer
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Spika, ninamshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa kuendelea kuwapigania ma-veteran hawa. Swali hili limeulizwa Wabunge wengi sana, mara kadhaa hapa Bungeni na nimekuwa nikilitolea majibu baada ya kuona kwamba majibu haya hayawaridhishi Wabunge. Kama Wizara tulifanya tathmini ya kina ili kuweza kujua tatizo ni nini. Kwa hiyo, tumekwishafanya tathmini ya kina kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha.
Mheshimiwa Spika, swali lake mahususi kwamba ni lini tutaleta marekebisho ya sheria, utaratibu uliopo ni kwamba mafao na stahiki za wanajeshi zinaongezwa na National Defense Act Cap. 192 ya Mwaka 2002 na Kanuni zake ambazo ni Defense Service Pension and Gratuity Regulations na hizi huwa zinakwenda kwenye halmashauri ya majeshi. Baada ya hapo inapelekwa kwa Amiri Jeshi Mkuu.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hatuleti hapa Bungeni, lakini tumekwishakamilisha taratibu zote. Halmashauri hiyo ya majeshi imeshakaa; nami ndiyo Mwenyekiti. Tumeshapitisha na tumeshawasilisha kunakotakiwa. Kwa hiyo, mara baada ya hapo basi tutaleta mrejesho tumefikia hatua gani.
Mheshimiwa Spika, ni suala ambalo tumetoa kipaumbele sana kwa sababu mara nyingi nimeulizwa swali hili na sisi tukaona kwamba tulifanyie kazi. Ninapenda sana kumshukuru Waziri wa Fedha kwa kutoa ushirikiano mkubwa sana ambao umetuwezesha kukamilisha uchambuzi na mapendekezo tuliyokuja nayo.
Mheshimiwa Spika, kuhusu mpango wa dharura; mpango wa dharura ndiyo huu tunaokwenda nao, lakini pale ambapo wapiganaji hawa (Ma-veteran) wanakuwa na shida mahususi za kidharura huwa hatuwaachi, tunawasaidia kadiri inavyotakiwa.
Mheshimiwa Spika, ninaomba kuwasilisha.
Name
Benaya Liuka Kapinga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbinga Vijijini
Primary Question
MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:- Je, lini Serikali itawalipa mafao yao mashujaa wa Vita vya Kagera na Uganda?
Supplementary Question 2
MHE. BENAYA L. KAPINGA: Mheshimiwa Spika, Serikali iko tayari kuwatambua hawa wazee na kujua hasa shida zao au malalamiko yao ni yapi na kuyafanyia kazi?
Name
Dr. Stergomena Lawrence Tax
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nominated
Answer
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Spika, tunawatambua na changamoto zao tumeshazifanyia tathmini na ndiyo maana katika jibu langu la msingi nimesema kwamba changamoto tulizoziainisha ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara ni kutaka kuingizwa kwenye Mfuko wa Pensheni kwa wale ambao hawakustahili.
Mheshimiwa Spika, changamoto ya pili ni matibabu na mapendekezo ndiyo tumekuja nayo waweze kupewa bima ya afya, lakini na hata wale ambao hawakustahili kupewa pensheni kwa hilo unalolisema kwa kutambua mchango wao tuone tunaweza kuwaingiza kwa namna gani. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved