Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Florent Laurent Kyombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkenge

Primary Question

MHE. FLORENT L. KYOMBO aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Uwanja wa Ndege Omukajunguti utaanza?

Supplementary Question 1

MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninashukuru sana na kuipongeza Serikali kwa kuwa juhudi za kujenga uwanja wa ndege ndani ya Wilaya ya Misenyi ambayo ulikuwa ni wa Omukajunguti ni za muda mrefu, lakini Serikali kama inavyosema kupitia Kamati maalumu iliweza kubaini eneo lingine ambalo ni karibu na eneo la awali la Omukajunguti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; wananchi ambao walikuwa katika maeneo ya Omukajunguti walisimamishwa kufanya shughuli za uendelezaji na za kiuchumi katika maeneo yao kwa muda mrefu na kimsingi walikuwa wameshafanyiwa na tathmini kulipwa fidia kupisha ujenzi wa uwanja wa ndege. Sasa, ni nini tamko la Serikali kwa wananchi hao kuhusiana na maeneo yao ili waweze kuyaendeleza katika shughuli zao za kiuchumi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa eneo la Kihabajwa linakaribiana na maeneo yanayomilikiwa na wananchi lakini mengine yanamilikiwa na Serikali zetu za vijiji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni nini mkakati wa Wizara yetu ya Uchukuzi kushirikiana na Wizara ya Ardhi na uongozi wa Mkoa na Wilaya ya Misenyi kuhakikisha kwamba tunafanya mipango miji vizuri kupima maeneo hayo, ili kuweza kuwa na maeneo ambayo yamepimwa ili kuleta kivutio pindi uwanja wa ndege utakapojengwa na maeneo ambayo yanazunguka uwanja huo yawe na yenyewe yana hadhi kama uwanja huu utakavyojengwa? Ahsante. (Makofi)

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nitumie nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Florent Laurent Kyombo, kwa maelezo yake mazuri aliyoyatoa ya kuipongeza Serikali yetu kwa jitihada ambazo tunazifanya, lakini ninampongeza kwa sababu ya uhamasishaji mkubwa ambao amekwishaanza kuufanya ikiwa ni pamoja na kuwaanda wananchi juu ya mradi mkubwa wa kiwanja cha ndege utakaojengwa katika eneo la Kihabajwa ambao haujawahi kutokea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni kazi nzuri ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye baada ya kuona umuhimu wa mkoa huo kiuchumi pamoja na sekta nyingine akaelekeza Wizara yetu kwamba, uwanja mnaotaka kuendelea kuuboresha hapana, ninataka ujengwe uwanja mkubwa utakaoendana na mahitaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lake la kwanza alilouliza, je wananchi wanaruhusiwa kuendeleza maeneo yao? Jibu ni ndiyo, kwa kuwa tayari tumeshakubaliana kwamba tutakwenda kujenga Kiwanja cha Ndege cha Kihabajwa, maana yake hili eneo la awali halitatumika tena kwa ajili ya jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lake la pili anauliza mpango wa Serikali. Ninapenda kumhakikishia na bahati nzuri nami nimekwenda eneo hilo nilikuwa na yeye mwenyewe na anafahamu kidogo. Sema hapa ninataka nchi nzima iweze kufahamu, tayari Serikali yetu kupitia Wizara ya Uchukuzi, ikishirikiana na Ofisi ya Mkoa kupitia Mamlaka yetu ya Viwanja vya Ndege, imekwishawasiliana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na kuanza mpango wa upimaji ili kuweza kuboresha eneo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo ni nini? Moja, ni kuhakikisha kwamba maeneo jirani na uwanja wa ndege yanakuwa na mandhari mazuri; lakini pili, kuvutia uwekezaji. Wote tunafahamu uwanja huu hautaishia kunufaisha watu wa Kagera tu, hata nchi jirani zitakwenda kuutumia uwanja huo. (Makofi)

Name

Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FLORENT L. KYOMBO aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Uwanja wa Ndege Omukajunguti utaanza?

Supplementary Question 2

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Ni lini ujenzi wa uwanja wa ndege wa Musoma utakamilika kwa maana ya run way pamoja na jengo la abiria ili kuweza kuanza kutumika na kukuza uchumi wa Mara kupitia utalii, biashara, pamoja na kurahisisha usafiri na usafirishaji? Ninakushukuru. (Makofi)

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza Mheshimiwa Matiko kwa sababu anavyokimbizana kufuatilia uwanja wa ndege wa Musoma, siyo muda mrefu atamkaribia mpaka Mbunge wa Jimbo la pale mjini jinsi anavyohangaikia usiku na mchana kuona kwamba uwanja huu unakamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie, kutokana na umuhimu mkubwa wa utalii, madini na maeneo mengine, Serikali iliamua kufanya maboresho ya uwanja wa Musoma na hivi ninavyozungumza umevuka asilimia 58 na mjenzi yupo site anaendelea na kazi baada ya kusimama kwa muda mrefu kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, ninamwomba aendelee kuwa na subira, Serikali ambayo imekwishaanza kujenga inakwenda kukamilisha uwanja huo wa Musoma. (Makofi)

Name

Daniel Awack Tlemai

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karatu

Primary Question

MHE. FLORENT L. KYOMBO aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Uwanja wa Ndege Omukajunguti utaanza?

Supplementary Question 3

MHE. DANIEL A. TLEMAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi. Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa uwanja wa Manyara Airport ili kuongeza utalii katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Manyara National Park?

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Awack kama alivyoliuliza. Anaulizia kuhusu uwanja wa ndege, ninafikiri anaongelea wa mkoa maana pale kuna viwanja viwili. Kama anazungumzia wa mkoa, tupo kwenye hatua za utoaji wa ardhi, tutakapozikamilisha Serikali itaanza kufanya taratibu za ujenzi. Kama anazungumzia ule wa utalii kwa maana ule wa Lake Manyara, tayari tumeshampata mkandarasi, tupo kwenye hatua za mobilization na ujenzi utaanza mara moja. (Makofi)

Name

Bonnah Ladislaus Kamoli

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Segerea

Primary Question

MHE. FLORENT L. KYOMBO aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Uwanja wa Ndege Omukajunguti utaanza?

Supplementary Question 4

MHE. BONNAH L. KAMOLI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kwanza ninachukua nafasi hii kuipongeza Serikali pamoja na Mheshimiwa Naibu Waziri. Nauliza Serikali, imewalipa wananchi 226 kati ya wananchi 1,800. Je, Serikali ina mpango gani kuwamalizia hawa wengine maana wapo kwenye hali mbaya na kuna mvua kubwa zinazonyesha? Ahsante. (Makofi)

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nitajibu kwa kifupi lakini moyo usio na shukrani hukausha mema yote. Ninampongeza Mheshimiwa Bonnah kwa kuweza kufuatilia na kupongeza Serikali hii kwa sababu jambo hili lilikwama kuanzia miaka ya 1990 ambapo wananchi zaidi ya 1,528 walikuwa wanadai. Tumekwishalipa shilingi bilioni 20 na siyo muda mrefu tutakwenda kulipa tena. Hii ni jitihada za Mheshimiwa Rais wetu na ninaamini kwa kuwa wameshaanza kulipa na hata waliobakia hao atakwenda kukamilisha. (Makofi)

Name

Edwin Enosy Swalle

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lupembe

Primary Question

MHE. FLORENT L. KYOMBO aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Uwanja wa Ndege Omukajunguti utaanza?

Supplementary Question 5

MHE. EDWIN E. SWALLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi hii. Kumekuwa na ahadi ya muda mrefu ya ujenzi wa uwanja wa ndege Mkoa wa Njombe na Mheshimiwa Naibu Waziri alikuja kwenye cave akaona lile eneo. Wananchi wetu wa Makambako, Njombe Mjini, Lupembe, kuna wafanyabiashara wengi sana, hata Mwenyekiti Mheshimiwa Deo Mwanyika ili apande ndege mpaka aende Mkoa wa Songwe au aje Mkoa wa Iringa, ni lini uwanja wa ndege Mkoa wa Njombe atajengwa sasa? (Makofi)

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilifikiri utaniambia nijibu kwa ufupi, lakini naona hujazungumzia hilo. Wewe na Mheshimiwa Swalle pamoja na Wabunge wote wa Mkoa wa Njombe, mmelifuatilia jambo hili kwa ukaribu sana na Serikali inatambua umuhimu wa uwanja wa ndege wa Njombe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali tulikuwa na mpango kwa ajili ya kukarabati ule uliopo, lakini baada ya kuona eneo ni dogo na mipango ni mikubwa, Serikali ikaona ni lazima ibadilishe uwanja ijenge uwanja mkubwa pengine wenye hadhi sawa na uwanja wa Songwe. Hii kwa sababu gani? Kwa sababu, kwanza unaweza kuona Mkoa wa Njombe ndiyo una maghala makubwa ya chakula ya NFRA. Mbili, tunao Mradi wa Liganga na Mchuchuma ambao tukikamilisha ujenzi wa reli ya kusini, uwanja ule ndiyo utakuwa jirani kwa ajili ya kufikisha watu mbalimbali kwenye eneo lile. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu, uwanja huo pia utakuwa na faida kubwa kwa kilimo cha parachichi pamoja na mazao mbalimbali, lakini pia yapo maeneo jirani ikiwa ni pamoja na Chimala ambapo pia kuna madini mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa uwanja huu, nimesema wiki iliyopita ninaomba nirejee tena, tumeshampata mkandarasi anaitwa Intercontinental Technocrats ambaye anafanya uhuwishaji, upembuzi yakinifu ili kuweza kujua gharama na mahitaji ya uwanja huo yatakuwaje. Hatimaye tukishamaliza hatua hiyo tutatangaza na tutampata mjenzi ajenge uwanja kama ambavyo yeye mwenyewe amekuwa akihitaji kwa muda mrefu. (Makofi)