Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Primary Question

MHE. STEPHEN L. BYABATO aliuliza: - Je, Serikali imeweka utaratibu gani wa kuwatambua wakandarasi wazawa wanaofanya kazi nzuri ili kuwapa motisha?

Supplementary Question 1

MHE. STEPHEN L. BYABATO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini ninalo swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bukoba Mjini tulipata pesa takribani shilingi bilioni 12.5 kwa ajili ya ujenzi wa njia nne kutoka katikati ya mji kwenda pembeni. Sasa napenda kufahamu, ni nini mkakati wa Serikali wa kuhakikisha inamuwezesha mkandarasi mzuri anayefanya kazi hiyo mzawa anayeitwa Abemulo Contractors kukamilisha kazi hiyo vizuri na kwa wakati ili na yeye tuweze kumpa pongezi, ahsante sana.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge Serikali itahakikisha kwamba kazi hiyo inakamilika ya kujenga njia nne na tuna kazi mbili pale, tuna miradi miwili, lakini mkandarasi ni huyo huyo. Kuna Mradi wa …. na huo mradi ambao unatekelezwa kwa fedha ya Serikali 100%.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulichokifanya sasa hivi, tumeshapeleka hati za madai kwa wenzetu wa Hazina ili aweze kuongeza kasi maana amerudi nyuma, aweze kuongeza kasi na kukamilisha kazi kwa sababu sasa hivi tupo kwenye 40%. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Bukoba, Serikali tutahakikisha kwamba hiyo hazi inakamilika, ahsante. (Makofi)

Name

Abeid Ighondo Ramadhani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Kaskazini

Primary Question

MHE. STEPHEN L. BYABATO aliuliza: - Je, Serikali imeweka utaratibu gani wa kuwatambua wakandarasi wazawa wanaofanya kazi nzuri ili kuwapa motisha?

Supplementary Question 2

MHE. ABEID R. IGHONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, naomba kujua ni lini sasa ujenzi wa Barabara ya Igauli – Ilongero kilometa kumi na moja na nusu zitaanza ujenzi wake?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, hii barabara iko kwenye majadiliano, tulishaitangaza, wakandarasi wameshapatikana, tuko kwenye majadiliano ya gharama za kuanza ujenzi kipande hicho cha Singida – Ilongero kilometa 11.5, ahsante. (Makofi)