Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Sebastian Simon Kapufi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpanda Mjini
Primary Question
MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI aliuliza:- Je, lini mnara wa mawasiliano wa kuongozea ndege utajengwa katika Uwanja wa Ndege Mpanda?
Supplementary Question 1
MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Ninalo swali moja la nyongeza. Kwa kuwa Uwanja wa Ndege wa Mpanda uko katika eneo zuri la kimkakati, kwa maana ya uchumi mpana ikiwa ni jirani na nchi ya DR-Congo. Serikali inasema nini kwa maana ya kuweka kwenye mipango yake uboreshaji wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, ikiwa ni pamoja na miruko na mituo sambamba na ujenzi huo wa mnara wa mawasiliano? (Makofi)
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba, kulingana na uhitaji wa mara kwa mara, Serikali imeendelea kujenga minara ya ndege katika maeneo mbalimbali hapa nchini, ikiwa ni pamoja na Viwanja vya Julius Nyerere, KIA, Arusha, Dodoma, Mwanza, Iringa, Tabora, Tanga, Mtwara, Songea na maeneo mengine, lakini kulingana na uhitaji mkubwa minara mbalimbali inajengwa kwa sababu ikiwa ni pamoja na Shinyanga, Sumbawanga, Kigoma, Tabora, Msalato na Iringa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo yako maeneo mengine ambayo tutaanza ujenzi sio muda mrefu, ikiwa ni pamoja na Tanga, Mtwara, Kigoma, Lindi na Lake Manyara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi, kama anavyofahamu Mheshimiwa Mbunge, Serikali imetumia fedha bilioni 1.4 katika Kiwanja cha Mpanda ambapo tumejenga runway, tumejenga jengo la abiria, tumejenga jengo la zimamoto na bado control tower.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepokea ushauri wa Mheshimiwa Mbunge ambao ametimiza jukumu lake la msingi la Kibunge ambalo ni kuishauri na kuisimamia Serikali na kwamba ushauri wake na hoja yake, itafanyiwa kazi kulingana na mahitaji, kama ambavyo nimeainisha hapo juu ikiwemo ni pamoja na miruko ya ndege, ratiba maalum zilizoko, tukiona inafaa kwa wakati husika tutalifanyia kazi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved