Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y. MHE. MWANTATU MBARAK KHAMIS aliuliza:- Je, kwa kiasi gani huduma za utengamao zinazotolewa na Wizara ya Afya zinasaidia watu wenye ulemavu kumudu maisha na kuleta maendeleo?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Maswali ya nyongeza ni mawili, tafadhali ninaomba leo Mheshimiwa Waziri ayajibu vizuri. Swali la kwanza; je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha huduma hizi zinatolewa katika hospitali za mikoa na kuhakikisha wataalam wanaongezeka?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; je, ni kiasi gani cha fedha kimetengwa kwa ajili ya huduma hizi unazozisema?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu maswali mawili ya mama yangu Dkt. Thea na nimhakikishie kwamba nitayajibu vizuri kabisa kama ambavyo tumekuwa tukiyajibu hata yaliyopita. Kwanza, nimwambie kwamba tunachokufanya ili kuhakikisha kwamba huduma hizi zinakwenda kwenye hospitali za mikoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie, kwamba kwenye hospitali za mikoa kuna huduma hizi; kwa kweli kama anavyosema, kwamba inahitaji kuboreshwa na kufanywa ya kisasa zaidi, ambapo sasa hivi ndiyo tumeelekeza fedha ili kuhakikisha kunakuwepo na kitengo maalum na idara maalum ambayo inahudumia masuala kama hayo. Kwa hiyo, hilo tunalizingatia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo tu suala la hospitali zetu za mikoa, pia kwenye hospitali za wilaya. Issue hapa, Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshatoa fedha kwa ajili ya eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, issue hapa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshatoa fedha kwa ajili ya eneo hilo ila sasa tunapambana na issue ya wataalam kwa sababu uzalishaji wa wataalam ni mdogo. Kwa hiyo, tunakosa wataalam wa kuweza kwenda kila wilaya, lakini kwa kweli ni eneo la kipaumbele na ni muhimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la pili, nimwombe dada yangu kama anaweza akarudia swali lake la pili.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Thea Ntara, jaribu kulifupisha swali la pili ili alielewe vizuri.

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeuliza ni kiasi gani cha fedha kimetengwa kwa ajili ya huduma hizo za utengemao?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri kama unajua kiasi; kama hujui unaweza kumwandikia kwa maandishi baadaye.

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachoweza kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge ni kwamba, kwa kweli fedha zimetengwa, lakini siwezi kumwambia specifically ni kiasi gani lakini ipo kwenye mpango. Kama alisikia bajeti ya mwaka jana hii bajeti tunayoitekeleza sasa katika vipaumbele 10 ambavyo vilitajwa na Wizara ya Afya, ninafikiri kipaumbele cha sita au cha saba ni suala la utengamao ni eneo ambalo limezingatiwa, likiwekwa pamoja na afya ya akili ambayo inaenda kwa pamoja. Kwa hiyo, imewekwa kama kipaumbele lakini fedha zimetengwa na mkakati na maelekezo mahususi ya Rais kwa ajili ya kuwekea uzito eneo hilo yapo tayari na yanatekelezeka.