Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza:- Je, lini Serikali itaweka uzio katika Hifadhi za Taifa ili kunusuru maisha ya wananchi na mali zao dhidi ya wanyamapori?
Supplementary Question 1
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu ya Serikali kwa kuwa maeneo yote yaliyotajwa hapo katika majibu ya Serikali hakuna maeneo ambayo yametaja Jimbo la Bunda, ninaomba kuwauliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; kwa kuwa Vijiji vya Hunyari, Kihumbu, Mariwanda, Sarakwa, Mugeta, Kyandege, na Tingirima vimeathirika sana na uharibifu wa wanyamapori na mazao yao yameathirika sana; je, ni lini sasa Serikali itaweza uzio katika vijiji hivyo? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa uharibifu umekuwa mkubwa sana na madai ya fidia ya kifuta machozi na kifuta jasho yamekuwa mengi sana katika Vijiji vya Hunyari, Kihumbu, Mariwanda, Sarakwa, Kyandege, Tingirima na Mugeta; ni lini sasa Serikali italipa kifuta machozi kwa wadai wa maeneo hayo? (Makofi)
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Getere, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo aliyoyataja yapo katika Mpango wa Serikali wa kuweka uzio katia ukanda huu. Zoezi hilo la kuweka uzio wa umeme lilikuwa limegawanyika katika mafungu matatu. Tumefanya utekelezaji katika fungu la kwanza, tulipokuwa tunataka kufanya uwekaji umeme katika fungu la pili kukatokea baadhi ya malalamiko kwa sababu, uzio ule ulikuwa unapita kwenye maeneo ambayo ni maeneo ya malisho ya wananchi. Kwa hiyo, inaonekana ni busara tusitishe kwanza zoezi hilo iundwe timu ya pamoja ambayo itafanya kazi ya kujenga uelewa wa pamoja vilevile kupitia maeneo haya, ili kuweka makubaliano na wananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, timu hii inatoa wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya TAMISEMI na Uongozi wa Mkoa na Wilaya katika maeneo haya. Timu hii imeanza kufanya kazi, ninamuomba Mheshimiwa Mbunge awe na subira. Tukikamilisha jambo hili tutaelekea awamu ya pili na ya tatu, ambayo itagusa maeneo haya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na ulipaji wa fidia. Tathmini imekwishafanyika kwa baadhi ya maeneo, ambayo taarifa zao zimefika. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, jambo hili linafanyiwa kazi, tunawasiliana na wenzetu wa Wizara ya Fedha, ili kuona jinsi ambavyo malipo haya yanaweza kufanyika hivi karibuni.
Name
Norah Waziri Mzeru
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza:- Je, lini Serikali itaweka uzio katika Hifadhi za Taifa ili kunusuru maisha ya wananchi na mali zao dhidi ya wanyamapori?
Supplementary Question 2
MHE. NORAH W. MZERU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipatia nafasi. Kutokana na tembo hao kuwa tishio kwa wananchi. Je, Serikali imejipangaje kuhakikisha haitetereki kwa namna yoyote juu ya usalama na amani wa nchi yetu tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba, 2025? (Makofi)
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo; usalama wa Watanzania ni kipaumbele chetu namba moja. Pamoja na kwamba, tunayo changamoyo hii, lakini Serikali imejizatiti kuhakikisha kwamba, maisha ya Watanzania yanalindwa kwa gharama yoyote ile. Nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, tumejipanga vizuri, tutahakikisha tunalinda maisha ya watu wetu.
Name
Edward Olelekaita Kisau
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kiteto
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza:- Je, lini Serikali itaweka uzio katika Hifadhi za Taifa ili kunusuru maisha ya wananchi na mali zao dhidi ya wanyamapori?
Supplementary Question 3
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Kwa miezi minne sasa tembo wameua wananchi zaidi ya wanne Kiteto, hata jana. Sasa ni lini utatuletea kikosi na helkopta kwa haraka sana, ili kuwafukuza wanyamapori warudi kwenye maeneo ya hifadhi? (Makofi)
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Olelekaita, kama ifuatavyo; ni kweli, tumekuwa na changamoto hii kwenye eneo la jimbo lake, amewasiliana na mimi kwa karibu na jana tulikuwa na mawasiliano. Hivi ninavyozungumza kikosi kipo njiani kuelekea kwenye jimbo lake. (Makofi)
Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza:- Je, lini Serikali itaweka uzio katika Hifadhi za Taifa ili kunusuru maisha ya wananchi na mali zao dhidi ya wanyamapori?
Supplementary Question 4
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Tunao mgogoro wa kati ya Wananchi wa Tarime Vijijini, Kata za Nyanungu, Goloma na Kwihancha na Hifadhi ya Serengeti. Mgogoro huo bado upo kwenye process, haujakamilika utatuzi wake. Mheshimiwa Waziri, kule wananchi wangu wa Nyanungu, Kwihancha na Karakatonga pale, wanapoenda kunywesha ng’ombe kwenye vyanzo mbalimbali vilivyo mpakani, ngo’mbe wanakamatwa, kutaifishwa na kupigwa faini kubwa. Serikali ipo tayari kuruhusu wananchi wangu waendelee kunywesha ng’ombe kwenye vyanzo vya maji vilivyopo sasa mpaka hapo mtakapochimba malambo, ili malambo yale wayatumie badala ya kwenda kugombana na wahifadhi? Ahsante.
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali moja la Mheshimiwa Mwita Waitara, kama ifuatavyo; zuio la kwenda kwenye maeneo haya ni kwa sababu kubwa ya uhifadhi na vilevile usalama wa nchi yetu. Nimwombe Mheshimiwa Mbunge, mara baada ya session hii ya asubuhi tukae, ili tuweze kutafuta suluhu ya pamoja ya jambo hili. (Makofi)
Name
Miraji Jumanne Mtaturu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Mashariki
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza:- Je, lini Serikali itaweka uzio katika Hifadhi za Taifa ili kunusuru maisha ya wananchi na mali zao dhidi ya wanyamapori?
Supplementary Question 5
MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaishukuru sana Serikali, katika Jimbo la Singida Mashariki tulipata uvamizi wa wanyama tembo, Mheshimiwa Naibu Waziri unajua, Waziri alifika na hatua ilichukuliwa kubwa ya kuleta kikosi. Miezi mitatu imepita sasa wale tembo wamerudi tena upya katika Kijiji cha Mkiwa na kusababisha usumbufu mkubwa. Ni nini hatua ya Serikali katika kupata suluhu ya kudumu ya hawa wanyama tembo wakakae kwenye hifadhi? (Makofi)
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mtaturu, kama ifuatavyo; ni kweli zimefanyika jitihada, lakini tembo wamerudi tena. Niwaelekeze wahifadhi wetu wapeleke kikosi kwa haraka, cha ndege nyuki, kwenda kudhibiti hali hiyo na baada ya hapo tuone njia nyingine mbadala ambazo tunaweza kuzitumia. (Makofi)
Name
Maimuna Ahmad Pathan
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza:- Je, lini Serikali itaweka uzio katika Hifadhi za Taifa ili kunusuru maisha ya wananchi na mali zao dhidi ya wanyamapori?
Supplementary Question 6
MHE. MAIMUNA A. PATHAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa kuuliza swali la nyongeza. Je, Serikali haioni haja ya kuchukua wazo lile ambalo nimekuwa nikilililia mara nyingi sana kuhusu kuweka uzio wa solar electric fence? (Makofi)
MWENYEKITI: Kuweka solar electric fence, wapi?
MHE. MAIMUNA A. PATHAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye maeneo ambayo yanazungukwa na Hifadhi za Taifa za Mbunga za Wanyama. (Makofi)
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Maimuna, kama ifuatavyo; kama ambavyo nimejibu kwenye swali la msingi, Serikali kwa sasa inafanya jambo hilo la kuweka uzio kwenye baadhi ya hifadhi, lakini utafiti wa kisanyansi umeonesha kwamba, hatuwezi kuweka uzio kwenye hifadhi zetu zote. Tunachofanya sasa ni kufanya utafiti wa kina kwenye maeneo ambayo yamepata athari kubwa ya wanyama hawa, ili tuweze kuona ni jinsi gani tunaweza kuyanusuru maeneo haya kwa kuyawekea uzio wa umeme.