Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Issaay Zacharia Paulo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Mjini

Primary Question

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza: - Je, ni hatua gani imefikiwa katika kutekeleza taarifa ya wataalamu kuhusu Ziwa Tlawi?

Supplementary Question 1

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maombi mawili. Ombi langu la kwanza ni kwamba, Serikali iweke muhimu mkubwa sana wa kutafuta fedha hizo ili kunusuru Ziwa Tlawi kwa kuwa bado lina mahitaji makubwa kwa wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu pamoja na maeneo mengine nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi la pili, namwomba Mheshimiwa Naibu Waziri, je, yupo tayari kwenda kutembelea ziwa hilo ili kuweka uzito wa jambo hili kwa umuhimu wake pamoja na hatua mbalimbali za haraka? (Makofi)
MWENYEKITI: Majibu, Mheshimiwa Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili sikulisikia vizuri naomba alirejee kidogo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Zacharia, swali la pili naomba ulirudie kwa uzuri.

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ni kwamba, je, Mheshimiwa Naibu Waziri yupo tayari kutembelea Ziwa Tlawi ili kuweka uzito wake kwa ajili ya jambo hili muhimu sana? (Makofi)

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ingawa moja limekuja kama ni ushauri, lakini nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari tumeshaanza mchakato wa kutafuta fedha na tayari tuna jumla ya miradi takribani 11 tumeshaiandikia. Miongoni mwa miradi hiyo ni miradi ya kusafisha mito, maziwa na maeneo mengine ambayo yameathirika kutokana na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo masuala ya magugu maji na kutuama kwa tope nzito.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie tu Mheshimiwa na Waheshimiwa wengine waendelee kuwa na subira, fedha zitakapopatikana, tutahakikisha kwamba tunaanzia maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kikubwa nimwambie Mheshimiwa Mbunge, kutokana na umuhimu wa jambo hili na udharura wake, nipo tayari kuambatana naye kwenda katika eneo hilo ili kuona hali ilivyo na kuona namna ambavyo tunaweza tukawasaidia wananchi, nakushukuru. (Makofi)

Name

Simai Hassan Sadiki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nungwi

Primary Question

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza: - Je, ni hatua gani imefikiwa katika kutekeleza taarifa ya wataalamu kuhusu Ziwa Tlawi?

Supplementary Question 2

MHE. SIMAI HASSAN SADIKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, shughuli za uvuvi, kilimo, ufugaji pamoja na usafirishaji na utalii zimekuwa zikitegemea sana vyanzo vya maji, lakini kiukweli kabisa kwa kipindi hiki kumekuwa na uharibifu mkubwa mno wa vyanzo vya maji. Je, ni upi msimamo wa Serikali katika kukabiliana na hali hii? (Makofi)

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Simai Sadiki, Mbunge na mtumishi wa wananchi wa Jimbo la Nungwi, kwamba ni kweli kumekuwa na changamoto ambayo inasababishwa na shughuli mbalimbali za kibinadamu ambazo zinaendelea kufanyika katika vyanzo mbalimbali vya maji na hasa ukiangalia katika maeneo ya bahari kwa maana ya maeneo ya ufukwe, yapo mambo yanafanyika huko zikiwemo shughuli za ulimaji wa mwani na shughuli nyingine za uvuvi usiyokuwa rasmi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba msimamo wa Serikali ni kwamba, tunawaomba sana wananchi waendelee kusimamia na kufuata sheria na taratibu zilizopo hasa hii sheria ya kuzingatia sheria ya umbali wa meta 60 kutoka usawa wa maji ili lengo na madhumuni tuweze kutunza na kuhifadhi vyanzo vya maji hasa maeneo haya ya bahari. Nakushukuru. (Makofi)

Name

Abdul Yussuf Maalim

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Amani

Primary Question

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza: - Je, ni hatua gani imefikiwa katika kutekeleza taarifa ya wataalamu kuhusu Ziwa Tlawi?

Supplementary Question 3

MHE. ABDUL YUSSUF MAALIM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali. Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa sasa, je, ni ipi kauli ya Serikali kutokana na uharibifu wa miundombinu, makazi na mali za wananchi wa Zanzibar? (Makofi)

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli mvua zinazoendelea, na kwa namna moja ama nyingine zimesababisha athari kubwa hasa ya maeneo ya makazi na kuharibika kwa baadhi ya miundombinu hasa kule Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie tu Mheshimiwa kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais tutaendelea kushirikiana, kuona namna ambavyo tunaweza tukawasaidia wananchi ili waweze kuepukana na mtihani huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo kubwa naomba kutoa wito kwamba wananchi waache kujenga na kuweka makazi yao katika maeneo ambayo yanatuama maji ili waweze kuepukana na mitihani hii hasa kipindi hiki ambacho mvua nyingi zinaendelea. Nakushukuru. (Makofi)