Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ally Abdulla Ally Saleh

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Malindi

Primary Question

MHE. ALLY SALEH ALLY aliuliza:- Yamekuwepo malalamiko mengi ya kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu wa kupiga watu, kuwatesa, kuchoma mali na kutishia amani katika Kisiwa cha Unguja Wilaya za Magharibi na Mjini na kwamba wahusika wamekuwa hawajulikani:- (a) Je, ni kwanini hali hiyo imeachwa kuendelea kwa muda mrefu? (b) Je, ni kwa nini Jeshi la Polisi limeshindwa kuwakamata wahusika? (c) Je, wananchi hao wategemee lini vitendo hivyo kutoweka?

Supplementary Question 1

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu yenye takwimu na hakikisho la usalama, lakini hivi sasa vitendo vya wale wanaoitwa mazombi na masoksi vinaendelea vikifanywa fawaisha kila siku na hata juzi watu kadhaa walipigwa katika Mtaa wa Kilimani na wengine wakapigwa katika Mtaa wa Msumbiji. Pia watu hawa wamekuwa wakiranda na silaha za moto, misumeno wa kukatia miti, wamekuwa wakivamia vituo vya redio, wamekuwa wakipiga watu mitaani. Swali langu la kwanza, je, kitu gani kinazuia kukamata uhalifu huu unaofanywa fawaisha kila siku na ambao unakuza culture of impunity katika nchi yetu?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, Serikali haioni vijana hao wanaoitwa mazombi wanaotumia magari ya KMKM ya KVZ, volunteer, magari ya Serikali waziwazi na namba zake zinaonekana kila kitu. Je, Serikali haioni kwamba kuruhusu hali hiyo kuendelea kunaitia doa Serikali katika suala zima la haki za binadamu na utawala bora? (Makofi)

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI: Mheshimiwa Naibu Spika, siku zote Jeshi la Polisi ama vyombo vya dola vimekuwa vikifanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi. Haya ambayo anazungumza Mheshimiwa Ally Saleh, nadhani amezungumza maneno mazombi, sijui ana maana gani, lakini ninachotaka kusema ni kwamba kama kuna uvunjifu wa sheria katika nchi yetu, basi taarifa hizi ziwasilishwe polisi na polisi itachukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.