Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Amb Dr. Diodorus Buberwa Kamala
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nkenge
Primary Question
MHE. BALOZI DKT. DIODORUS B. KAMALA aliuliza:- Msitu wa Hifadhi ya Taifa Minziro una vivutio vingi vya utalii. (a) Je, ni watalii wangapi wametembelea msitu huo ndani ya kipindi cha miaka 20 hadi sasa? (b) Je, wananchi wanaoishi karibu na msitu huo wananufaikaje?
Supplementary Question 1
MHE. BALOZI DKT. DIODORUS B. KAMALA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, huo mpango unaoandaliwa ni jambo jema na kwa kuwa mpango huo utatusaidia vijiji vinavyozunguka maeneo hayo kupata asilimia 26, ni lini maandalizi ya mpango huo yatakamilika? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa katika kata hiyo ulipo Msitu wa Minziro kuna kitongoji kinaitwa Bulembe na kwa kuwa katika kijiji hicho kuna ngome zilizotumiwa na Wajerumani kupigana Vita ya Pili ya Dunia na kwa kuwa katika eneo hilo huwezi kwenda kwa sababu hakuna barabara isipokuwa uwe jasiri kutumia pikipiki au kutembea kwa miguu zaidi ya saa sita, je, Waziri au Naibu Waziri yuko tayari kuandamana nami kutembea zaidi ya saa sita kwenda kuona vivutio hivyo? (Makofi)
Name
Eng. Ramo Matala Makani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduru Kaskazini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa umesema kwa ufupi ni kwa ufupi kwa sababu na maswali yenyewe yalikuwa yanaelekeza kupata majibu kwa ufupi. Kuhusu swali lake la kwanza, lini mpango utakamilika, mpango huu utakamilika ndani ya mwaka wa fedha uliokwishaanza.
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, je, Waziri au Naibu Waziri yuko tayari kuandamana naye kwenda kuona vivutio alivyovitaja ambavyo viko ndani ya msitu lakini pia ni vivutio vya malikale.
Mheshimiwa Spika, jibu lake ni kwamba mimi au Mheshimiwa Waziri wakati wowote ule tutakapokuwa tumepata fursa na hasa baada ya kikao hiki cha Bunge tutakuwa tayari kwenda kuona na tutaweza kuona namna gani tunaweza tukaondoa changamoto hiyo ya miundombinu ambayo ni mojawapo ya changamoto zinazosumbua kwenye sekta ya utalii.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved