Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Faida Mohammed Bakar
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FAIDA MOHAMMED BAKAR aliuliza:- Je, ni lini Serikali itatenga bajeti kwa ajili ya kuwajengea nyumba askari polisi wa Pemba ili kuwaondolea adha ya makazi askari hao?
Supplementary Question 1
MHE. FAIDA MOHAMMED BAKAR: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza.
Kwanza napenda kuishukuru Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi kwa kusikia kilio cha askari wetu wa Tanzania, wakiwemo askari wa kule Pemba kwa kuwatengea bajeti kwa mwaka 2018/2019 ya kuwajengea nyumba. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali imekiri na kukubali na kuweka ahadi kwamba itatenga bajeti hiyo ya kuwajengea askari wa Zanzibar nyumba. Je, Mheshimiwa Waziri atakubaliana na mimi kwamba bajeti hiyo ikitengwa na nyumba hizo zitakapoanza kujengwa kipaumbele kipewe kwa askari wetu wa Mkoa wa Kusini Pemba? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Iramba Magharibi
Answer
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Faida Bakar, kwa kweli ni balozi wa askari wote hapa nchini kwa kuwasemea vizuri sana kuhusu mahitaji yanayowahusu kwenye mahitaji yao na Waheshimiwa wengine wanaokuwepo kwenye Kamati inayosimamia mambo ya ndani akiwemo Mheshimiwa Masoud.
Mheshimiwa Spika, nakubaliana tutaweka kipaumbele hicho cha askari walioko Pemba na mimi nilishafika kwa kweli mazingira yao ni magumu ya kufanyia kazi kwa kukosa nyumba. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved