Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. BONIPHACE M. GETERE (K.n.y. MHE. AMINA N. MAKILAGI) Aliuliza:- Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma katika Kata za Etaro, Ifulifu, Nyegina na Nyakatende wanakabiliwa na taizo la maji. Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapatia wananchi wa kata hizo maji safi na salama?

Supplementary Question 1

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri, lakini hili tatizo la hizi kata limekuwa la muda mrefu na hasa ukizingatia kwamba kata zenyewe ziko pembezoni mwa Mji wa Musoma. Nataka kuuliza ni lini haya maji yatawafikia hizo kata kwa sababu wamekuwa na usumbufu wa muda mrefu?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, pamoja na matatizo ya mji wa Musoma pia kuna matatizo makubwa ya Mji wa Bunda na hasa Jimbo la Bunda ninakotoka mimi. Kuna kata saba zina matatizo makubwa ya uhaba wa maji ambazo ni Unyali, Kitale, Mgeta, Mihingo, Nyamaghunta na Salama; nilitaka kumuomba tu Waziri ni lini atafika? Nimuombe tu afike kwenye hizo kata saba za Jimbo langu ili aweze kujionea hali halisi ya uhaba wa maji katika jimbo hilo? Ahsante sana.

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; ni kweli kwamba, ni muda mrefu, lakini nimuahidi kwamba, mara mradi huu ambao umeanza kutekelezwa utakapokamilika wakazi hawa watafaidika na maji hayo. Swali la pili kuhusu Bunda; naomba nimuahidi Mheshimiwa Mwita Getere kwamba mara baada ya Mkutano huu wa Bunge nitatembelea Mkoa wa Mara na nitafika Bunda. Ahsante sana.