Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Deogratias Francis Ngalawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ludewa

Primary Question

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA aliuliza:- Wafanyakazi wa TTCL wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliolipwa pesheni ni wale waliofungua kesi mahakamani na kushinda. Aidha, wapo ambao wanastahili malipo lakini hawakuwa na uwezo wa kumlipa Wakili katika kuendesha kesi hiyo. Je, ni lini Serikali itawalipa wafanyakazi wa TTCL wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki madai ya pesheni zao?

Supplementary Question 1

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Ukijaribu kuangalia suala hilo jinsi lilivyo, hawa wote walikuwa wanastahili kulipwa lakini kilichotokea ni kwamba wenzao walikuwa na uwezo wakaajiri advocate na kwenda mahakamani.
Je, Serikali haioni busara kwa sababu kesi hiyo ni kama inawahusisha wote isipokuwa tu hawa wengine hawakuwa na uwezo wa kumpata advocate kwamba hata hawa wakienda mahakamani watalipwa sawa na kama ambavyo wenzao wamelipwa?

Name

George Mcheche Masaju

Sex

Male

Party

Ex-Officio

Constituent

None

Answer

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ngalawa kwamba majibu ya Naibu Waziri katika swali lake la msingi amesema msingi wa malipo yale na hawawezi wakalipa kwa madai ambayo hayajathibitishwa kisheria. Natambua pia kwamba hawa wafanyakazi wamemuomba Waziri wa Katiba na Sheria kusudi wapate fursa ya kufungua mashauri. Kama wanataka kufanya ambavyo wenzao walifanya basi wafungue kesi, lakini Serikali haiwezi kulipa tu madai ambayo hayajathibitishwa kisheria.