Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jaku Hashim Ayoub
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
House of Representatives
Primary Question
MHE. JAKU HASHIM AYOUB aliuliza:- Tarehe 25/5/2017 Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi akijibu swali Na. 274 kuhusu madai ya mkandarasi aliyejenga vituo vya polisi Mkokotoni Unguja na Madungu alisema, deni tayari limeshahakikiwa na kwamba atalipwa mara fedha zitakapotolewa lakini huu ni mwaka wa tano deni hilo halijalipwa:- (a) Je, Serikali ina nia thabiti ya kumlipa mkandarasi? (b) Je, Serikali inasubiri ipelekwe Mahakamani ndipo ilipe deni hilo? (c) Je, huu ndiyo utawala bora ambao nchi yetu ina dhamira ya kuujenga?
Supplementary Question 1
MHE. JAKU HASHIM JAKU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Naibu Waziri na Waziri wake kwa majibu yao ya umakini kabisa. Naomba kuuliza maswali madogo tu ya nyongeza yenye fungu (a) na (b):-
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika majibu yako Mheshimiwa Naibu Waziri, swali la msingi umesema Waziri amesema katika mwaka wa fedha 2017/2018 Jeshi la Polisi limetenga jumla ya shilingi bilioni 2.2 kwa ajili ya kupunguza madeni ya wakandarasi waliotekeleza miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa ujenzi wa huu wa Kituo cha Mkokotoni. Umetenga shilingi milioni 200 na kutenga maana yake ni kitu tayari umekiweka pembeni na huyu mtu ni mgonjwa, hili suala nimelisemea karibu mara nne katika chombo hiki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini nije naye mguu kwa mguu ili asije akapata usumbufu apate haki yake hii, ili akamalize kituo hiki na yeye mwenyewe apate matibabu?
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, kwa vile deni hili lina muda mrefu kwa nini, Serikali au Wizara haitoi priority ikammalizia deni hili, ili kumaliza ujenzi huu wa vituo vyetu vilivyokuwa huko Unguja na Pemba? Ahsante sana.
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue fursa hii kwa niaba ya Serikali kumpa pole sana huyu mkandarasi kutokana na maradhi ambayo ameyapata na tunamuombea Mwenyezi Mungu amjalie aweze kupona haraka. Nimuombe sana Mheshimiwa Mbunge hana haja ya kumhangaisha mkandarasi kuja naye hapa mguu kwa mguu, asiwe na wasiwasi wowote fedha hizi shilingi milioni 200 zimetengwa kwa ajili yake katika bajeti ya mwaka huu na kwa hiyo basi, fedha hizo zitakapokuwa zimeingia tu atalipwa bila hata kumsumbua mkandarasi kwa kuja naye hapa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili kwamba lisiwe kipaumbele. Ni kipaumbele na ndiyo maana tukatenga hizo fedha kwa ajili ya kumlipa. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge tunaomba vile vile awe na subira wakati tukisubiri fedha hizi wakati zitakapokuwa zimeingia na tutamlipa mara moja.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved