Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Selemani Jumanne Zedi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukene
Primary Question
MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza:- Je, Serikali kupitia REA inachukua hatua gani kwa Mkandarasi CHICCO ambaye ameshindwa kukamilisha utekelezaji wa Mradi wa Kupeleka Umeme Vijijini Awamu ya Pili (REA II) katika vijiji vya Mwangoye, Mbutu na Mambali?
Supplementary Question 1
MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Bukene, nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa ziara ambayo aliifanya katika Jimbo hili hivi karibuni na vijiji vyote vilivyotajwa kwenye swali hili vya Mwangoye, Mambali na Mbutu, Mheshimiwa Naibu Waziri alivipitia na kutoa maelekezo maalum kwa TANESCO, REA na CHICCO…
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Zedi, naomba uulize swali tafadhali.
MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Naibu Spika, sasa swali langu ni kwamba kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi katika kijiji cha Mwangoye, Mambali na Mbutu, jambo ambalo limefanya wananchi wengi kufanya wiring na kuwa tayari na fedha ya kulipia, lakini kuna upungufu mkubwa wa nguzo na vifaa vya kuunganishia.
Mheshimiwa Naibu Waziri anaweza kutumia forum hii kutoa agizo au kauli maalum kwa watendaji wa REA, TANESCO na CHICCO kuhakikisha kwamba wananchi wote wa Mwangoye, Mambali na Mbutu ambao wameshajiandaa kupata umeme wanapatiwa nguzo na vifaa vya kuunganishiwa ili waweze kupata huduma muhimu ya nishati?
Name
Dr. Medard Matogolo Kalemani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chato
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda tu niongeze maelezo kwenye shukrani alizotoa na mimi namshukuru sana Mheshimiwa Zedi kwa pongezi na shukrani za kuunga mkono. Nampongeza sana pamoja na wananchi wa Bukene. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niende kwenye swali lake, kimsingi siyo swali lakini anataka wananchi wake wapate uhakika. Ni kweli kabisa nguzo zinaendelea kwenda Bukene katika vijiji vyote vitatu na katika mwezi ujao wananchi wapatao 50 watapatiwa umeme kwa sababu nguzo wameshapelekewa.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved