Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Joseph Leonard Haule
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Mikumi
Primary Question
MHE. JOSEPH L. HAULE aliuliza:- Wanyama hasa Tembo wamekuwa wakiharibu sana mazao ya wananchi kwa fidia ndogo sana ya Sh. 20,000 kwa heka na hii hupunguza ushiriki wa wananchi katika kuzuia ujangili ndani ya Hifadhi:- Je, Serikali imejipangaje kukaa vizuri na wananchi wa vijiji vinavyopakana na Hifadhi ili kuwa na ushirikiano katika kuzuia ujangili?
Supplementary Question 1
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza nisikitishwe sana na majibu haya ya Serikali ambayo wamekuwa wakiyajibu mara kwa mara, kiukweli yanakatisha sana tamaa. Kwa sasa huu utaratibu wa Serikali wanaosema ni kifuta jasho kwa wananchi ambao wanakuwa wameuliwa na tembo au mazao yameharibiwa kiukweli haina uhalisia na haileti haki kwa wananchi ambao wamekaa kwenye mazingira hayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, hii yote inatokana na sheria ya wanyamapori ambayo imeonekana kuwa na usumbufu na upungufu mkubwa sana. Ni lini Serikali itaileta sheria hii hapa Bungeni ili iweze kubadilishwa ili iweze kwenda na uhalisiana kurudisha fidia na hili neno la kifuta jasho libadilishwe iwe fidia iliyokuwa imetathiminiwa kutokana na matatizo ambayo wamepata wananchi? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili juzi kuamkia jana katika Kijiji cha Kikwaraza pale Mikumi ambapo Mbunge wa Mikumi anaishi, simba alivamia zizi la mfugaji anaitwa Agrey Raphael na kuua ng’ombe mmoja pamoja na kujeruhi ng’ombe wawili.Sasa hayo matatizo na changamoto kama hizi zimekuwa nyingi sana kule Mikumi kwenye Kata kama Mikumi, Luhembe, Kidodi, Kilangali, pamoja na maeneo ya Mhenda. Je, Naibu Waziri yuko tayari kuambatana na mimi kuelekea kule mikumi ili akasikilize changamoto nyingi za wananchi ambao wamekuwa na kilio cha muda mrefu kutokana na matatizo kama haya ya wanyamapori kabla hawajaamua kuchukua sheria zao mikononi kwa kutumia silaha za jadi? Ahsante. (Makofi) [Maneno haya siyo sehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge)
Name
Jenista Joackim Mhagama
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Peramiho
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii naomba….
Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara yangu iko sasa hivi inafanya kuiisha tunapitia upya sera na sheria pamoja na taratibu mbalimbali ambazo zinatumika katika kutoa hiki kifuta jasho na machozi, ni hivi karibuni tu tutaileta hii sheria hapa ndani Bungeni ili Bunge lako Tukufu liweze kushauri na liweze kuipitisha.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali la pili la kuambatana naye, nataka nimwambie tu niko tayari mara baada ya shughuli za Bunge kukamilika, nitaambatana naye kwenda kuangalia maeneo hayo yote yalioathirika. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved