Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Desderius John Mipata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkasi Kusini

Primary Question

MHE. DESDERIUS J. MIPATA aliuliza:- Wananchi wa Kata ya Nkandasi wamejitahidi kujenga shule ya Sekondari ya Kata ya Milundikwa hadi kufikia kidato cha sita lakini Serikali kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imeamuru shule hiyo kuhamishwa mara moja kuanzia tarehe 1 Januari, 2017 kuachia Jeshi:- (a) Wananchi walitumia muda na rasilimali zao kukamilisha ujenzi huo na sasa wanakwenda kuanza upya: je, ni upi mchango wa Wizara kwa ujenzi mpya wa shule? (b) Wizara ya Elimu imeafiki kuhamishwa shule hiyo ya Kata; Je, ni upi mchango wa Wizara katika uhamishaji wa shule hiyo? (c) Je, Serikali iko tayari kufanya uthamini wa miundombinu yote ya shule na majengo, yaliyojengwa na wananchi na thamani hiyo kuitoa katika fedha taslimu kwa ujenzo wa shule mpya?

Supplementary Question 1

MHE. DESUDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana na nichukue nafasi hii kutambua juhudi kubwa sana na kuipongeza Serikali kwa kazi nzuri waliyoifanya kwenye shule hii, lakini pia usimamizi mzuri uliotolewa na Mkuu wetu wa Wilaya na kwa hakika nimeridhika sana na majibu ya Serikali, lakini hata hivyo nina maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; shule hii ni ya bweni kwa kidato cha tano na cha sita. Haina nyumba ya matron wala haina uzio wa ulinzi wa wanafunzi. Naomba Serikali itoe hela zaidi kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na huduma ya vijana hawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Halmashauri ilijitahidi kuchimba kisima cha maji lakini kiko mbali kidogo na shule. Naomba Serikali itoe pesa zaidi kwa ajili ya kusogeza maji kwa ajili ya huduma ya wanafunzi hawa. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nampongeza Mheshimiwa Mipata na Mheshimiwa Keissy, wilaya yao ni miongoni mwa wilaya zinazoongoza katika ujenzi wa madarasa. Mwaka jana peke yake wamejenga madarasa 550 ambayo yanatakiwa kuezekwa sasa hivi. Kwa hiyo nawapongeza sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili hitaji la kwanza alilosema la nyumba ya matron, uzio; nilifika pale Milundikwa, nimeona kweli ni mahitaji halisi nayo tutayafikiri kadri ambavyo tunapata uwezo wa kifedha lakini kwa kushirikiana na halmashauri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili kuhusu kisima, shule ya sekondari ya Milundikwa tumeiingiza kwenye orodha ya shule 100 ambazo zitapata ufadhili wa fedha kutoka kwa Sultan Qaboos wa Oman. (Makofi)

Name

Frank George Mwakajoka

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Tunduma

Primary Question

MHE. DESDERIUS J. MIPATA aliuliza:- Wananchi wa Kata ya Nkandasi wamejitahidi kujenga shule ya Sekondari ya Kata ya Milundikwa hadi kufikia kidato cha sita lakini Serikali kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imeamuru shule hiyo kuhamishwa mara moja kuanzia tarehe 1 Januari, 2017 kuachia Jeshi:- (a) Wananchi walitumia muda na rasilimali zao kukamilisha ujenzi huo na sasa wanakwenda kuanza upya: je, ni upi mchango wa Wizara kwa ujenzi mpya wa shule? (b) Wizara ya Elimu imeafiki kuhamishwa shule hiyo ya Kata; Je, ni upi mchango wa Wizara katika uhamishaji wa shule hiyo? (c) Je, Serikali iko tayari kufanya uthamini wa miundombinu yote ya shule na majengo, yaliyojengwa na wananchi na thamani hiyo kuitoa katika fedha taslimu kwa ujenzo wa shule mpya?

Supplementary Question 2

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mji wa Tunduma ni mji unaokuwa sana na una msongamano mkubwa sana wa watoto; na mwaka wa jana Waheshimiwa Madiwani kwa kushirikiana na wananchi waliweza kuanzisha shule mpya nane ambazo zingine zina madarasa matatu, zingine zina madarasa nane lakini shule hizi mpaka sasa hivi hazijaanza kutumika kwa sababu DC amewasimamisha Madiwani. Kwa, hiyo kuna baadhi ya shughuli ambazo zilitakiwa zifanyike kama vioo na mambo mengine hayajafanyika kwa sababu wananchi pia walikuwa wanategemea Madiwani. Je, ni lini Serikali itatia mkazo kuhakikisha kwamba Madiwani wanarudi kazini ili shule hizi zianze kutumika haraka iwezekanavyo? Ahsante sana.

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Halmashauri ilijitahidi ikajenga shule nane na hizi shule hazijaanza kutumika, ni kweli; lakini ni matokeo ya migogoro ambayo haina sababu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana wenzetu wa Halmasahuri ya Mji wa Tunduma walipokaa kwenye kikao cha rasmi walikataa ushirikiano wa aina yoyote na Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya. Sasa hilo likawa ni chanzo cha matatizo ambayo yamesababisha Waheshimiwa Madiwani wasiweze kutimiza majukumu yao. Suala lao tunalishughulikia kitaifa na namwahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba tutalitatua hivi karibuni, ili kusudi waweze kuendelea kutekeleza majukumu yao kama kawaida. (Makofi)