Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Musa Rashid Ntimizi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Igalula

Primary Question

MHE. MUSA R. NTIMIZI aliuliza:- Wananchi wa Kata ya Loya katika Halmashauri ya Tabora (Uyui) wameitikia wito wa Serikali wa ulinzi kwa kujenga kituo kikubwa cha polisi katika kata yao:- (a) Je, ni lini kituo hicho kitafunguliwa hasa ikizingatiwa kuwa Loya ni zaidi ya kilometa 120 kutoka Makao Mkuu ya Wilaya Isikizya ambako ndiko kwenye kituo cha polisi? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaongezea bajeti ya mafuta ili kuwarahisishia watendaji kazi maana maeneo ya Jimbo ni kubwa na yote yanahitaji huduma za kipolisi?

Supplementary Question 1

MHE. MUSA R. NTIMIZI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, nina maswali madogo mawili ya nyongeza.
Wananchi wa Jimbo la Igalula hususani Kata ya Loya na Halmashauri yetu imefanya kazi kubwa sana kujenga kituo hicho cha polisi na nguvu kwa sasa imetuishia na kazi kubwa imefanyika. Serikali kupitia Wizara haioni umuhimu wa kusaidia nguvu hizi za wananchi katika kumalizia kituo hiki cha polisi na kiweze kuanza kufanya kazi? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, katika Kata ya Igalula na Kata ya Kigwa kuna vituo vya polisi ambavyo vingeweza kutoa huduma katika Kata ya Loya kipindi hiki hatuna kituo kituo cha polisi katika Kata ya Loya. Tatizo letu kubwa lililopo pale katika vituo hivi viwili vya polisi havina usafiri. Je, Wizara haioni umuhimu wa kuvipa usafiri vituo hivi vya polisi ili viweze kuendelea kutoa huduma katika maeneo ambayo hayana vituo vya polisi?

Name

Charles Muhangwa Kitwanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali bado inaendelea na juhudi zake za kuhakikisha kwamba inajenga vituo mbalimbali katika nchi yetu. Kwa hiyo basi, pamoja na juhudi zilizofanywa na wananchi, nimwombe Mheshimiwa Mbunge ashirikiane na Serikali na kuona kwa namna gani tunaweza tukakamilisha kituo hiki. Nina uhakika kabisa wananchi kwa juhudi walizozifanya bado kuna nafasi ya kuendelea kushirikiana na Serikali ili kukamilisha ujenzi huo.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili amezungumzia tatizo la usafiri. Ni kweli vituo vingi havina usafiri lakini Serikali katika bajeti yake ya mwaka huu inajipanga kuhakikisha kwamba inanunua magari mengi ili kuweza kuvipatia vituo mbalimbali usafiri na tutaangalia kituo kimojawapo kati ya alivyovisema tutaweza kukipatia usafiri.

Name

Savelina Slivanus Mwijage

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MUSA R. NTIMIZI aliuliza:- Wananchi wa Kata ya Loya katika Halmashauri ya Tabora (Uyui) wameitikia wito wa Serikali wa ulinzi kwa kujenga kituo kikubwa cha polisi katika kata yao:- (a) Je, ni lini kituo hicho kitafunguliwa hasa ikizingatiwa kuwa Loya ni zaidi ya kilometa 120 kutoka Makao Mkuu ya Wilaya Isikizya ambako ndiko kwenye kituo cha polisi? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaongezea bajeti ya mafuta ili kuwarahisishia watendaji kazi maana maeneo ya Jimbo ni kubwa na yote yanahitaji huduma za kipolisi?

Supplementary Question 2

MHE. SAVELINA S. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa kuwa kituo cha Chalinze ni kituo ambacho kiko kwenye barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma na kituo hicho hakina computer hata photocopy hakuna.
Kwa hiyo, ukipata tatizo wanaenda kutoa photocopy nje kwenye stationery. Ni lini Serikali itaona umuhimu wa kuwawekea photocopy machine ya kuwa wanatumia kuliko kusambaza nje siri za kituo hicho?

Name

Charles Muhangwa Kitwanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, juzi tu Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo hilo alinipigia simu, tuliongea naye na hayo anayosema Mheshimiwa Mbunge tuliyazungumza. Kwa hiyo, asiwe na wasiwasi ajue kwamba na Mbunge wa Jimbo hilo ameshanieleza tatizo hilo na tutalitatua.