Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Primary Question

MHE. MWITA M. WAITARA (K.n.y MHE. JOHN W. HECHE) aliuliza:- Mazingira ya ufundishaji kwa Walimu walio wengi nchini ikiwemo Wilaya ya Tarime yamekuwa siyo rafiki, ambapo Walimu wamekuwa wakibebeshwa mzigo wa gharama za vifaa vya kufundishia kama maandalio ya somo, chaki na kadhalika:- Je, matumizi haya yatarekebishwaje katika mfumo huu wa elimu bure ulioanzishwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Supplementary Question 1

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Pamoja na majibu ya Serikali ningependa niulize maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; pamoja na maelezo haya bado Walimu hao wameendelea kuchangishwa michango na kwa sababu wanaowachangisha ni mabosi wao ikiwemo michango ya mwenge na Mwalimu asipokubali kuchanga michango anawajibishwa kule kwa sababu Waziri hayupo. Je, ni hatua gani zinachukuliwa kwa wakubwa wa Walimu hawa kwa maana ya Wakuu wa Idara za Elimu, Maafisa Elimu kama wataendelea kuwachangisha michango ya lazima kinyume na maelekezo ya Serikali? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, jambo la pili, kwa jibu hilo la Mheshimiwa Waziri ni wazi tunafahamu kwamba kuna waraka ulitembezwa ambao unatoa maelekezo, lakini baada ya maelekezo ya Mheshimiwa Rais ilizuka sintofahamu na wananchi walikuwa wamechanga vyakula katika mashule mbalimbali wakaanza kugawana, kuna miradi ya kuchangia madawati, madarasa na kuta mbalimbali wakaanza kukataa. Je, ni hatua gani za dharura kwa Serikali ili kutoa maelekezo kwa wananchi na wadau mbalimbali wa elimu warudi kama zamani washirikiane Walimu na walezi wa shule hizi ili shughuli za maendeleo ziendelee kuwepo kwa maana ya kuondoa kero za elimu katika maeneo mbalimbali? (Makofi). Mheshimiwa Spika, ahsante.

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, baadhi ya michango halali kwa mfano michango ya Mwenge inatakiwa ichangishwe kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya na sio vinginevyo. Hii michango haitakiwi kupitia kwenye Kamati za Shule wala mikutano ya wazazi katika shule, hiyo hairuhusiwi. Kwa hiyo, Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ndiyo inayoratibu masuala yote yanayohusu Mwenge michango ikiwepo michango ya mwenge.
Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili kuhusu sintofahamu ya michango iliyosababisha baadhi ya watu kwenda kudai michango ambayo walikuwa wamechanga hapo awali. Napenda nisisitize msimamo wa Serikali kwamba ilikuwa ni makosa hapo mwanzo tulivyokuwa tunachangisha kwa kuwahusisha Walimu kuwaondoa darasani wanafunzi kwa sababu tu wazazi wao labda kwa sababu ya umaskini wao hawakuwa wamechanga. Hilo lilikuwa ni kosa kwa sababu mtoto yule aliyekuwa anatolewa darasani hakuwa na kosa lolote.
Mheshimiwa Spika, maelekezo ya Mheshimiwa Rais yanasimama pale pale, isipokuwa utaratibu ambao sasa hivi tumeupitisha katika kutekeleza ule Waraka Na.5 wa Elimu kuhusu michango ni kwamba michango yote sasa itaratibiwa na Serikali za Vijiji na Kata chini ya usimamizi wa Mkurugenzi wa Halmashauri.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Serikali ya Kijiji, Halmashauri ya Kijiji ikikutana ikapendekeza, wanapeleka kwenye Mkutano Mkuu wa Kijiji, wakikubaliana wanapeleka maamuzi yao kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata ambayo ikipitisha inapeleka kwa Mkurugenzi, Mkurugenzi anatoa idhini ya mchango ule kuchangwa. Mchango ukishachangwa ukikamilika taarifa inatolewa kwa Mkurugenzi ili hatua zaidi za utekelezaji ziendelee. Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.