Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Justin Joseph Monko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Kaskazini

Primary Question

MHE. JUSTIN J. MONKO aliuliza:- Mradi wa REA Awamu ya Pili katika Jimbo la Singida Kaskazini ulisimama tangu mwaka 2016 na kukosesha huduma hiyo kwa vijiji vilivyokusudiwa mwaka 2017, utekelezaji wa REA Awamu ya Pili katika vijiji 30 kati ya 64 vilivyokusudiwa umeanza. (a) Je, ni nini kauli ya Serikali juu ya ukamilishaji wa mradi wa REA II? (b) Je, ni lini mkandarasi wa REA II awamu ya pili atapatikana na kuanza kazi?

Supplementary Question 1

MHE. JUSTIN J. MONKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Singida Kaskazini lina Kata 21 na Vijiji 84. Kata za Muhunga, Ngimu, Itaja, Makulo na Ughandi hazina kijiji hata kimoja ambacho kimepitiwa na miradi ya umeme wa REA II na REA III. Je, ni lini wananchi hawa watapata fursa hiyo ya kupata umeme ambao ni muhimu sana katika shughuli za maendeleo? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mradi wa REA Awamu ya Tatu ambao umeshaanza sasa yapo maeneo ya wananchi ambayo tayari wameshajiandaa pamoja na taasisi ambayo yanarukwa na umeme, katika mpango wa upatikanaji wa umeme huu ambao unaendelea sasa. Serikali ina kauli gani kwa wananchi katika maeneo hayo ambayo tayari wameusubiri umeme huu kwa muda mrefu na wako karibu na njia za umeme? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Subira Khamis Mgalu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Napenda nimpongeze sana Mheshimiwa Monko, ni Mbunge mgeni lakini kwa kipindi kifupi cha kuchaguliwa kwake amefanya kazi kubwa ya kufuatilia miradi ya nishati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa kiti chako pia kimekuwa kikiagiza mara kwa mara kupitia Mheshimiwa Spika na Waheshimiwa Wenyeviti na Naibu Spika, naomba niliarifu Bunge lako tukufu kwa miradi yote ya REA kwa ujumla yake, kulikuwa na agizo la kufuatilia ufunguaji wa Letter of Credit.
Naomba niliarifu Bunge lako tukufu na niishukuru Kamati ya Bajeti, Wizara ya Fedha na Benki Kuu na nikutaarifu kwamba mpaka sasa Wizara ya Nishati kupitia REA tumefanikiwa kufungua Letter of Credit kwa makampuni 14 yenye jumla ya shilingi bilioni 220. Hii maana yake nini? Maana yake ni kwamba kuanzia sasa utekelezaji wa miradi ya REA Awamu ya Tatu itapata kasi kubwa. Niwathibitishie Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote kwamba wategemee sasa miradi kushika kasi kubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nijielekeze kwa maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, swali lake la kwanza ametaja Kata kadhaa ambazo amesema amesema hakuna hata Kijiji kimoja ambacho kina umeme katika REA zote zilizopita mpaka sasa. Nimthibitishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kwa kweli kwa mradi huu unaoendelea wa REA awamu ya tatu, mzunguko wa kwanza na mzunguko wa pili yatafikiwa maeneo yote. Kwa hiyo, maeneo na kata ambazo amezitaja zitapatiwa umeme katika mzunguko wa pili utakaoanza Julai, 2019 na kukamilisha Juni, 2021. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, katika maeneo ambayo Mradi wa REA umeanza, Mheshimiwa Mbunge amesema zipo taasisi za umma zimerukwa na yapo maeneo ambayo wananchi wamepitiwa na umeme mkubwa lakini hawana dalili za kupata umeme.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimthibitishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Wizara ya Nishati imetoa maelekezo kwa wakandarasi wote nchi nzima. Hapa namwomba mkandarasi wa Mkoa wa Singida na wakandarasi wote; na kama nilivyosema sasa mambo ni mazuri, wahakikishe kazi inakwenda kwa mujibu wa scope na yale maeneo ambayo yameainishwa yapate huduma hii. Ahsante. (Makofi)