Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Stephen Hillary Ngonyani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Korogwe Vijijini
Primary Question
MHE. STEPHEN H. NGONYANI aliuliza:- Katika Kata ya Magoma, Korogwe Vijijini kumejengwa Mahakama ya Mwanzo ya Kisasa, lakini toka ijengwe imefika miaka saba sasa haijafunguliwa:- Je, ni lini Serikali itafungua Mahakama hiyo ili wananchi waachane na usumbufu wa kufuata huduma za Mahakama Korogwe?
Supplementary Question 1
MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa majibu mazuri ya Profesa mwenzangu. Naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuwa Tarafa ya Magoma ina Kata Nane na katika Kata hizi ina Mahakama moja tu ya Mwanzo ambayo ni hiyo ya Mashewa na huu mradi umechukua muda mrefu bila kufunguliwa. Nataka Serikali iniambie ni tarehe ngapi Mahakama hii itakuwa imefunguliwa?
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, maneno anayoelezwa hapo Mheshimiwa Waziri, naomba kama kutakuwa na uwezekano aende. Hayo anayoambiwa kwenye karatasi yanalingana na jinsi Mahakama yenyewe inavyotengenezwa kule nilipo? Nitaomba twende wote ili akahakikishe, aone kwamba imechukua muda mrefu, wanafanya kazi bila kudhibiti na tunapata usumbufu sana kwa walalamikaji na washtakiwa kwenda zaidi ya kilometa 35. (Makofi)
Name
Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilosa
Answer
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Kata ile inahitaji Mahakama zaidi na naamini katika mpango utakaofuata wa maendeleo wa miaka 10 wa Mahakama baada ya huu unaoisha 2020 kukamilika, tutatazama tena maeneo ambayo Kata zao ni kubwa na Mahakama ni chache ili katika mpango huo wa awamu ya pili wa ujenzi wa Mahakama nchini maeneo hayo yaweze kuangaliwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la pili la kutembelea eneo la Mashewa ili kujionea jinsi Mahakama hiyo inavyojengwa, niko radhi kufika huko na sina wasiwasi Profesa kwa sababu na mimi mjomba wangu ni fundi kama wewe, kwa hiyo nitafika na kuondoka salama. (Kicheko)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved