Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Bhagwanji Maganlal Meisuria
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chwaka
Primary Question
MHE. BHAGWANJI MAGANLAL MEISURIA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka gari, radio call pamoja na vitendea kazi vingine katika Kituo cha Polisi cha Chwaka na Jozani?
Supplementary Question 1
MHE. BHAGWANJI MAGANLAL MEISURIA: Mheshimiwa Spika, nampongeza Naibu Waziri amesema maneno mazuri naunga mkono. Hata hivyo, nataka nimwambie wananchi wa Jimbo langu la Chwaka wana matatizo vilevile. Wabakaji wengi na watu mbalimbali wanakuja kufanya uhaini katika Jimbo langu huko Chwaka na Jozani. Mimi mwenyewe nimeshachangia computer moja Jozani lakini nimeomba gari mbili angalau hata moja ipatikane kwa sababu hali ni ngumu na ni lazima tupate gari moja kwa heshima na taadhima.
Mheshimiwa Spika, ni hayo tu, naomba Serikali na Waziri wanipatie gari gari moja ya Polisi ili liweze kusaidia wananchi wa Jimbo langu. Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:
Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Bhagwanji, Mbunge wa Chwaka, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimejibu swali la msingi kwamba mchakato utakapokamilika wa upatikanaji wa magari kwa kuzingatia vigezo ambavyo nilivyovieleza tutaangalia kuona kama Chwaka inakidhi vigezo hivyo na idadi ya magari yaliyopo ili tupeleke. Nimuombe Mheshimiwa Mbunge avute subira mpaka magari hayo yatakapokuwa yamepatikana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved