Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jaku Hashim Ayoub
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
House of Representatives
Primary Question
MHE. JAKU HASHIM AYOUB aliuliza:- Benki Kuu ya Tanzania (BOT) inalo jukumu la kuzisimamia benki nyingine hapa nchini pamoja na kulinda haki za wateja wa benki za biashara. Kwa zaidi ya miaka miwili sasa Benki ya FBME imefungwa kwa sababu ya ukiukwaji wa sheria za kifedha na mpaka sasa jambo hilo halijapatiwa ufumbuzi. (a) Je, ni sababu gani inayofanya benki hiyo isiwalipe wateja wake haki zao au amana zao? (b) Je, Serikali haioni kuwa BOT imeshindwa kutimiza wajibu wake wa kuzisimamia benki nyingine na kuwafanya wananchi kukosa imani na mifumo ya kibenki inayorudisha nyuma utaratibu wa kuhifadhi fedha? (c) Je, Serikali haioni kuwa tunakosa mapato ambayo yangetusaidia kwa ajili ya maendeleo ya nchi?
Supplementary Question 1
MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nimkumbushe tu kidogo Mheshimiwa Naibu Waziri kwa vile alikuwa ni mwalimu wangu kullu-kum rai, wakullu-kum mas-ul alayhi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, waliokuwa wafanyakazi wa benki ambayo waliondolewa kazini na wasimamizi wa Deposit Insurance Board (DIB) ndio wakasimamia ufilisi wa benki hiyo. Hawajalipa wafanyakazi hao mpaka sasa hivi na ukizingatia ni wapiga kura wetu, ni wananchi wetu kwa muda mrefu sasa hivi. Je, haioni sheria hiyo aliyoitaja kuwa imepitwa na wakati na inawakandamiza wananchi na lini ataleta sheria hiyo? That is (a).
Mheshimiwa Mwenyekiti, ya pili katika majibu yake alisema kukusanya madeni pamoja na fedha za benki zilizopo kwenye benki nyingine nje ya nchi na kulipa amana za benki, nataka nimwambie tu FBME correspondence bank ni Dutch Bank hebu tuambie kiasi gani ambazo ziko huko na lini zitaletwa ili wananchi hao na Serikali kukosa mapato. Na hivi juzi tumeshuhudia makontena kupigwa mnada wananchi wanataka kununua makontena hayo ili wapate biashara?
Name
Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Kondoa
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la kwanza ni swali la wafanyakazi wa iliyokuwa Benki ya FBME. Napenda kuliarifu Bunge lako tukufu kwamba, taratibu za wafanyakazi zinashughulikiwa na sheria za kazi za Taifa letu. Kwa hiyo, wafanyakazi wale walipoajiriwa na benki hii walisaini mikataba na hivyo sheria za kazi za Taifa letu zinaendelea kusimamia haki ya wafanyakazi wote waliokuwa wa benki hii ya FBME.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la pili napenda kumwambia Mheshimiwa Jaku Hashim kwamba avute subira tunaendelea kufuatilia kama anavyofahamu yeye kwamba benki hii ilikuwa ni benki ambayo asilimia 10 ya uendeshaji wake ulikuwa ndani ya Taifa letu na asilimia 90 ulikuwa nchini Cyprus. Kama Wizara na Benki Kuu tunaendelea kulifuatilia jambo hili kwa ukaribu na tunawahakikishia wateja wetu watapata fedha zao kwa muda muafaka.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved