Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Oran Manase Njeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbeya Vijijini

Primary Question

MHE. ORAN M. NJEZA (K.n.y. MHE. HAROON M. PIRMOHAMED) aliuliza:- Je, ni lini Serikali itafanyia ukarabati barabara za Mahongole – Kilambo kilometa 20, Igurusi – Utengule kilometa 22, Chimala – Kapunga kilometa 25 na Mlangali – Ukwavila kilometa 23?

Supplementary Question 1

MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana na vilevile nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali lakini ningependa kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, kutokana na ajali nyingi zinazotokea katika Wilaya ya Mbeya na hasa katika Milima ya Uyole na Mbalizi. Je, ni lini Serikali itafanya upanuzi wa barabara zinazoelekea kwenye nchi za jirani za Zambia na Malawi?
Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itajenga by pass ya Inyala – Simambwe na Inyala – Songwe? Nashukuru sana.

Name

Elias John Kwandikwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza niseme kwamba study zilizofanyika zinaonyesha kuwa ajali nyingi zinazotokea asilimia 78 zinatokana na makosa ya kibinadamu (human behavior) na asilimia 12 iliyobaki ndiyo inasababishwa na mambo mengine ikiwepo miundombinu. Kwa ajali ambazo zinatokea katika Mkoa wa Mbeya niseme tu ajali iliyotokea juzi kwa mfano nimepata fursa ya kuwepo Mbeya juzi, eneo ajali ilipotokea ni eneo ambalo barabara ni nzuri na alama za barabarani zipo, inawezekana lilikuwa tatizo la kiufundi lakini tu kwa ujumla wake Serikali imechukua hatua ya kuendelea kuboresha barabara za Mbeya kwa sababu nature ya eneo la Mbeya ni milima na miteremko mirefu ili kuweza kupunguza ajali kwa maana kwamba ile barabara sasa anayoitaja Mheshimiwa Mbunge Inyala – Simambwe ni kati ya barabara ambazo tunaendelea kufanya usanifu ili tuweze kupunguza ule msongamano mkubwa wa magari.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kwa ujumla wake tu ninapende kutoa wito kwa watumiaji wa barabara kwamba maeneo haya ambayo yanakuwa na milima mikali na alama za barabarani zipo, watumiaji wa magari tuzingatie hizo kanuni za barabarani ili tupunguze ajali wakati Serikali inafanya juhudi za kuboresha barabara zake. Kwa hiyo, tatizo la Mbeya niseme kwa ujumla Serikali inalitambua na tunafanya haraka kuhakikisha kwamba tunaboresha miundombinu na kupunguza ajali katika eneo hili.