Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Daimu Iddi Mpakate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kusini

Primary Question

MHE. DAIMU I. MPAKATE aliuliza:- Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ina jumla ya kata 39 na vijiji 157. Halmashauri iliomba kuigawa Wilaya hiyo ambayo ina ukubwa zaidi ya Mkoa wa Mtwara wenye Wilaya sita:- (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuigawa Wilaya ya Tunduru ili iwe rahisi kutoa huduma karibu zaidi na wananchi? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuzigawa Kata za Mchoteka, Mtina, Namasakala, Lukumbule, Mchasi, Tuwemacho na Misechela ambazo zina wakazi zaidi ya 30,000 kila Kata? (c) Je, Serikali itaidhinisha lini mgao wa vijiji uliopendekezwa na Halmashauri mwaka 2015 ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi?

Supplementary Question 1

MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri aliyotoa Naibu Waziri, nina maswali mwili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, katika jitihada hizo za kuimarisha maeneo yaliyokuwepo sasa kuna tatizo la Watendaji Kata maeneo mengi katika Jimbo la Tunduru Kusini na Tunduru kwa ujumla walio wengi wanakaimu.
Je, Serikali itapeleka lini watendaji wa kudumu ambao wameajiriwa katika nafasi ya Kata, Vijiji na Katibu Tarafa?
Swali la pili, kwa kuwa majukumu mengi yaliyopo kwa sasa Vijijini yanafanywa na Watendaji wa Vijiji wakishirikiana pamoja na Wenyeviti wa Vijiji; na kwa kuwa Halmashauri nyingi zimeshindwa kutoa posho kwa maana ya asilimia 20 kwenye Vijiji husika.
Je, Serikali haioni haja kwa sasa kutoa posho kwa viongozi wa vijiji kwa maana ya Wenyeviti wa Vijiji ili waweze kufanya majukumu yao vizuri? (Makofi)

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba katika nchi tunao upungufu mkubwa wa Watendaji wa Kata, kwa kweli siyo Watendaji wa Kata peke yake bali kada nyingi na Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha kwamba tunamaliza au tunapunguza kwa kiasi kikubwa upungufu wa watendaji wetu katika kada mbalimbali. Kwa upande wa Watendaji wa Kata, mwaka jana tuliajiri nafasi chache lakini mwaka huu tunao mpango wa kuajiri Watendaji wa Kata 1,000 nchi nzima. Ninaamini watakapoajiriwa hao watapunguza sana upungufu wa uwepo wa Watendaji Kata katika Kata nyingi hapa nchini ikiwemo Kata za Wilaya ya Tunduru.
Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili kwamba Watendaji wa Vijiji na Wenyeviti wa Vijiji ndiyo wanaofanya kazi kubwa huko kwenye vijiji vyetu. Napenda nikubaliane sana na Mheshimiwa Daimu Mpakate kwamba ni kweli Wenyeviti wa Vijiji na Wenyeviti wa Vitongoji wanafanya kazi kubwa kwa kuwaongoza vizuri watendaji wa vijiji walioko huko kufanya kazi za Serikali kwa niaba ya wananchi.
Mheshimiwa Spika, amesema kwamba posho hawapati, natoa hapa agizo ambalo lilishatolewa na Serikali tayari kwamba suala la kushusha asilimia 20 ya mapato ya ndani kupeleka kwenye Kata, Vijiji na Vitongoji kwa ajili ya posho za Waheshimiwa Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji, hilo ni suala la kikanuni na kisheria.
Kwa hiyo Wakurugenzi wa Halmashauri ni lazima watekeleze agizo hilo kikamilifu. Pale ambapo tutagundua kwamba mtu hatekelezi kwa sababu tu ya ujeuri au ukaidi itabidi tuchukue hatua za kiutawala na kiutumishi. Kuna wale ambao ni Wakurugenzi wanapata shida kidogo kutokana na makusanyo hafifu, tunawaomba sana Mabaraza ya Madiwani waridhie mapendekezo ya wataalam kuhusu kupanua wigo wa vyanzo vya mapato ya ndani ambavyo vitasaidia kuweza kupatikana fedha ambazo hatimaye zitapelekwa kwa viongozi hawa kwa ajili ya posho.

Name

George Malima Lubeleje

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Primary Question

MHE. DAIMU I. MPAKATE aliuliza:- Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ina jumla ya kata 39 na vijiji 157. Halmashauri iliomba kuigawa Wilaya hiyo ambayo ina ukubwa zaidi ya Mkoa wa Mtwara wenye Wilaya sita:- (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuigawa Wilaya ya Tunduru ili iwe rahisi kutoa huduma karibu zaidi na wananchi? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuzigawa Kata za Mchoteka, Mtina, Namasakala, Lukumbule, Mchasi, Tuwemacho na Misechela ambazo zina wakazi zaidi ya 30,000 kila Kata? (c) Je, Serikali itaidhinisha lini mgao wa vijiji uliopendekezwa na Halmashauri mwaka 2015 ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi?

Supplementary Question 2

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali imesitisha ugawaji wa maeneo makubwa yakiwemo Majimbo pamoja na Wilaya, lakini kuna Kata moja iko mlimani inaitwa Kata ya Mkanana, hata Mheshimiwa Spika unaifahamu ni milimani hasa. Makao Makuu ya Kata yako kilometa 50 wanateremka kusikiliza mikutano. Je, Serikali inasemaje kuhusu Kata hii ya Mkanana na Chibwegere ili wazigawe? Wananchi wanapata shida sana kusafiri.

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Spika, ni kweli kama alivyosema, tumesitisha, lakini kulingana na umuhimu na mahitaji ya muda maalum, kama ambavyo tumepitisha uanzishwaji wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kuutangaza Mji wa Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi kwa sababu ni mahitaji maalum kwa muda maalum, kwa suala hili la Kata ya Mtanana kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge amelieleza vizuri sana hapa Bungeni na kwa sababu anawawakilisha wananchi wake ambao anaamini wanapata shida kwenda kwenye Makao Makuu ya Kata kilometa 50, namuagiza Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa kesho aende Mtanana na timu yake ya wataalam ili watuletee mapendekezo yao.