Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Primary Question

MHE. JUMA OTHMAN HIJA aliuliza:- Katika Jimbo la Tumbatu kumekuwa na matukio ya uvunjifu wa amani kwa wananchi wanaoishi katika kisiwa hicho na katika hali ya namna hiyo inaporipotiwa kwa Jeshi la Polisi inakuwa tabu kwenda kwa haraka kwenye eneo husika kwa sababu kadhaa ikiwemo ya ukosefu wa usafiri:- Je, Serikali haioni umuhimu wa kujenga Kituo cha Polisi katika kisiwa hicho na kuwapatia usafiri wa uhakika kwa kuzingatia jiografia ya maeneo hayo?

Supplementary Question 1

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri napenda kumuuliza swali moja la nyongeza:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza katika majibu yake ya msingi anasema kwamba, Serikali imepata kiwanja! Sijui maana yake ni nini kwa sababu hicho kiwanja ni chetu watu wa Jimbo, siyo Serikali! Pamoja na hayo mpaka sasa hivi hatuoni dalili za uharaka wa ujenzi wa suala hili. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri anatuambia ni lini angalau wataanza kuweka msingi katika suala hilo?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tuna dhamira ya dhati ya kujenga hiki kituo, lakini kama ambavyo nimezungumza mwanzo kwamba, tuna changamoto nyingi sana za mahitaji ya vituo mbalimbali. Kwa hiyo, ningechukua fursa hii kutoa wito kwa Waheshimiwa Wabunge, akiwemo Mheshimiwa Mbunge wa Tumbatu, kuangalia uwezekano wa kuharakisha jitihada hizi kwa kuanza kushirikisha wananchi na hata ikibidi kutumia Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo ili baadaye Serikali iweze kuongeza nguvu zake.

Name

Masoud Abdalla Salim

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Mtambile

Primary Question

MHE. JUMA OTHMAN HIJA aliuliza:- Katika Jimbo la Tumbatu kumekuwa na matukio ya uvunjifu wa amani kwa wananchi wanaoishi katika kisiwa hicho na katika hali ya namna hiyo inaporipotiwa kwa Jeshi la Polisi inakuwa tabu kwenda kwa haraka kwenye eneo husika kwa sababu kadhaa ikiwemo ya ukosefu wa usafiri:- Je, Serikali haioni umuhimu wa kujenga Kituo cha Polisi katika kisiwa hicho na kuwapatia usafiri wa uhakika kwa kuzingatia jiografia ya maeneo hayo?

Supplementary Question 2

MHE. MASOUD ABDALLA SALIM: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja dogo la nyongeza. Pamoja na maelezo ya Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba, kuna mkakati wa kupeleka Polisi
NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)
18
kwenye Kisiwa cha Tumbatu siku hadi siku kukabiliana na matatizo ya usalama, lakini Mheshimiwa Naibu Waziri bado hujatueleza ni mkakati gani wa ziada wa kuweza kuwabaini na kuwakamata wale ambao walifanya uhalifu wa kuchoma moto nyumba za watu kule Tumbatu, ambapo hadi sasa watu wengine wamekosa makazi. Je, kuna mkakati gani wa Waziri na Serikali kuhakikisha kwamba, matatizo yale hasa yanaepukwa na hayatokei tena na yanakoma na wahusika wanakamatwa? Naomba maelezo!

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, siku zote Jeshi la Polisi limekuwa likichukua hatua kadri ya matukio ya uhalifu yanapotokea ikiwemo tukio la uhalifu ambalo limetokea Tumbatu. Kuna mambo mawili makubwa ambayo tumefanya tayari, la kwanza, ni kuhakikisha kwamba, tunachukua hatua kwa wale ambao tumewakamata, watuhumiwa kwa ufupi kwa kuwapeleka katika vyombo vya sheria.
Mheshimiwa Naibu Spika, hatua ya pili, ni kudhibiti hali ile isijitokeze tena, ndiyo maana katika jibu langu la msingi nilizungumza kwamba kumeongezeka doria na sasa hivi nadhani kwa kipindi kirefu kidogo, matukio yale ya uhalifu ya kuchomeana moto nyumba yamepungua ama yamesita Tumbatu.