Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rwegasira Mukasa Oscar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Primary Question

MHE. OSCAR R. MUKASA aliuliza:- Wananchi wa Kijiji cha Luganzu na majirani zao wa Ntumagu wanakabiliwa na adha kubwa ya matukio ya ujambazi pamoja na ukosefu wa Kituo cha Polisi kijijini hapo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi. Je, Serikali inatoa kauli gani kuhusu hali hiyo?

Supplementary Question 1

MHE. OSCAR R. MUKASA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na namshukuru Naibu Waziri kwa majibu lakini naomba nipeleke pongezi kwa wananchi wa Kijiji cha Luganza na Ntumagu kwa sababu ni nguvu zao za wananchi za ujenzi wa kituo hicho ambazo ndio zimesababisha utulivu, nina maswali mawili.
Ni lini Serikali Wizara itajenga nyumba za askari kwasababu hivi tunavyozungumza askari wanne na familia zao wanaishi ndani ya kituo, kwa hiyo, kuna muingiliano wa minong’ono na mazungumzo baina ya familia za askari na mahabusu hasa nyakati za usiku? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili ni lini Serikali itatoa usafiri walau pikipiki kwasababu eneo hili kijiografia limekaa kwa namna ambayo askari wale wanahitaji usaidizi zaidi wa namna ya kufika kwenye maeneo wanayohudumia? (Makofi)

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na suala la nyumba kama ambavyo nimekuwa nikijibu katika siku za karibuni kwamba kuna jitihada mbalimbali ambazo zimefanyika ambazo zinahusisha pia Mkoa wa Kagera kwa ujumla pamoja na Wilaya ya Biharamulo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Mkoa wa Kagera tunakumbuka kwamba kuna nyumba ambazo zimefikia takribani asilimia 75 kukamilika pale Buekera ambazo katika bajeti ya mwaka huu tunatarajia kuzikamilisha, lakini sambamba na hilo katika fedha ambazo Mheshimiwa Rais ametupatia hivi karibuni za ujenzi wa nyumba 400 basi maeneo hayo yatahusika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na suala la gari ni kweli kuana changamoto ya usafiri lakini tumefanya jitihada kupeleka magari nadhani kama ni manne sasa hivi kwa mkoa wa Kagera kwa ujumla na kipaumbele chetu kimeelekea zaidi katika maeneo ambayo yako mpakani ili kudhibiti uhalifu hasa kwa wahamiaji haramu ambao wamekuwa wakiingia na kufanya uhalifu katika nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nichukue changamoto hii katika eneo lake ambapo tuna magari katika kituo hiki ambacho nimekitaja cha Nyakanazi tuna gari mbili zinasaidia kufanya doria katika maeneo ya kituo hiko, hata hivyo tunakubaliana na ombi la Mheshimiwa Mbunge kwamba kuna haja ya kuongeza pale ambapo magari yatapatikana tutaongeza vilevile kulingana na changamoto ya hali ya mahitaji mengine nchi nzima.