Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Susan Limbweni Kiwanga
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Mlimba
Primary Question
MHE. SUSAN L. KIWANGA aliuliza:- Jimbo la Mlimba lina vijana wengi wanaomaliza elimu ya msingi na sekondari na vyuo lakini wanashindwa kujiajiri kwa kukosa elimu ya ufundi kutokana na jimbo kuwa na kituo kimoja cha ufundi stadi kilichopo Shule ya Msingi Mchombe. Hata hivyo, kituo hicho chenye mahitaji ya walimu sita kina walimu wawili pekee na hakina vifaa. Aidha, kituo kilichopo Shule ya Msingi Mpanga hakina walimu wala vifaa:- (a) Je, ni lini Serikali itaboresha vituo hivyo vya Mchombe na Mpanga kwa kuwapelekea walimu na vifaa? (b) Vijana wachache wanaomaliza Kituo cha Mchombe na kufanya mitihani ya NECTA hawapewi vyeti. Je, ni lini Serikali itaweka utaratibu mzuri katika vituo hivyo ili wawe wanapewa vyeti ili waweze kujiendeleza katika vyuo vya Serikali na kupata madaraja? (c) Kwa kuwa mitaala ya vyuo vingi imepitwa na wakati, je, Serikali haioni haja ya kuboresha mitaala ya vituo hivyo ili iendane na wakati uliopo kama vyuo vya VETA?
Supplementary Question 1
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, kama unavyoona hilo jibu la Serikali, nadhani hili linawagusa Wabunge wote. Ni hivi wameweka vituo vya ufundi, wanafunzi wanakwenda kule wanafundishwa lakini wakimaliza hawapewi cheti hata kimoja. Hivi hii ni halali kweli? Hii ni Tanzania nzima. Je, kwa nini Serikali mnawafanyia hivi watoto wa maskini wa nchi hii? Lini mtaanza kuwapa vyeti? Darasa la saba wanapewa vyeti, kwa nini wanaoenda ufundi hamuwapi vyeti ili waweze kujiendeleza? Kama si dhuluma ni nini kwa watu maskini? Hilo ni swali kwanza, Waheshimiwa Wabunge wote linawahusu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili, sawa wamesema hiyo inatiwa LGCD kwa maana ya grants. Bunge zima linajua mwaka huu hamna hata shilingi iliyokwenda na Waziri wa Fedha ameshindwa kujibu. Je, hiyo milioni shilingi 10, shilingi 15 mna uhakika gani itakwenda wakati shilingi bilioni 1.5 Wilaya ya Kilombero mpaka sasa mwaka unakaribia kwisha hawajapeleka hata senti 5. Kwa nini Serikali isiwe na mpango maalum na hii ni nchi ya viwanda kupeleka hizo pesa ili vituo hivi vya Mpanga na Mchombe viendelee kuliko kutegemea hiyo grants? Hakuna kitu hapa, hapa tunadanganyana tu, mimi nataka kujua lini mnapeleka hizo hela?
Name
Joseph George Kakunda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Sikonge
Answer
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA):
Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge wa Mlimba kwamba tuko makini na wasikivu na ndiyo maana katika majibu yangu kwenye swali la msingi nimemwambia tumeupokea ushauri wake kikamilifu kwa ajili ya kuufanyia kazi.
Mheshimiwa Spika, kwanza, kwa sababu mafunzo haya katika vituo hivi ni mapya. Kweli mtalaa ni wa muda mrefu lakini tulikuwa hatuutumii, tumeanza kuutumia mwaka 2015 kwenye vituo hivi 208, tumepata mafunzo mazuri sana ya kutosha na tutakapoanza kutoa vyeti tutatoa vyeti vyote mpaka kwa wale ambao walisoma kuanzia mwaka 2015. Mwakani tutaanza kutoa vyeti, ndiyo maana nimesema tumechukua ushauri wake kwa ujumla kwa ajili ya kuufanyia kazi.
Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili, mimi sipendi sana kuwa mtabiri kutabiri mwaka 2018/2019 utakuwaje. Nimhakikishie kwamba hizi fedha ambazo tumezitaja katika jibu letu la msingi zitaenda wala asiwe na wasiwasi wowote.
Name
Margaret Simwanza Sitta
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Urambo
Primary Question
MHE. SUSAN L. KIWANGA aliuliza:- Jimbo la Mlimba lina vijana wengi wanaomaliza elimu ya msingi na sekondari na vyuo lakini wanashindwa kujiajiri kwa kukosa elimu ya ufundi kutokana na jimbo kuwa na kituo kimoja cha ufundi stadi kilichopo Shule ya Msingi Mchombe. Hata hivyo, kituo hicho chenye mahitaji ya walimu sita kina walimu wawili pekee na hakina vifaa. Aidha, kituo kilichopo Shule ya Msingi Mpanga hakina walimu wala vifaa:- (a) Je, ni lini Serikali itaboresha vituo hivyo vya Mchombe na Mpanga kwa kuwapelekea walimu na vifaa? (b) Vijana wachache wanaomaliza Kituo cha Mchombe na kufanya mitihani ya NECTA hawapewi vyeti. Je, ni lini Serikali itaweka utaratibu mzuri katika vituo hivyo ili wawe wanapewa vyeti ili waweze kujiendeleza katika vyuo vya Serikali na kupata madaraja? (c) Kwa kuwa mitaala ya vyuo vingi imepitwa na wakati, je, Serikali haioni haja ya kuboresha mitaala ya vituo hivyo ili iendane na wakati uliopo kama vyuo vya VETA?
Supplementary Question 2
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kunipa na mimi niulize swali la nyongeza, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, suala la mafunzo ya ufundi ni muhimu sana vijijini, sana, kwa hiyo naunga mkono kwa kweli suala la kuhimiza uimarishaji wa utoaji wa elimu ya ufundi vijijini, kwa sababu wengi hawaendelei na kidato cha kwanza na hata wanaomaliza kidato cha nne hawana mahali pa kwenda. Je, Serikali ina mpango gani wa kuimarisha hivyo vituo alivyokuwa anazungumzia Mheshimiwa Susan lakini pia FDCs ili viweze kutoa ufundi unaotakiwa? Ahsante sana.
Name
William Tate Olenasha
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ngorongoro
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYASI NA TEKNOLOJIA:
Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Margaret Sitta, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ni kweli kama anavyosema Mheshimiwa Mbunge kwamba kuna umuhimu mkubwa sana wa kuhakikisha kwamba tunaendeleza elimu ya ufundi nchini. Naomba tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali imejipanga kuhakikisha kwamba tunaboresha mazingira ya elimu ya ufundi. Kwa kuanzia kama alivyouliza, katika bajeti ambayo wametupitishia ya mwaka unaokuja, Wizara ya Elimu itakarabati vyuo 30 vya FDCs, vile vyuo vya wananchi, kati ya 55 vilivyopo. Tumetenga zaidi ya shilingi bilioni 10 kuhakikisha kwamba vile vyuo vinakarbatiwa lakini tunajaribu kuangalia mahitaji yao ya wafanyakazi ili kuhakikisha kwamba sasa vinafanya kazi katika hali nzuri zaidi.
Mheshimiwa Spika, vilevile naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika azma hiyo hiyo ya kujaribu kuendeleza elimu ya ufundi, Wizara yangu inatekeleza mradi wa unaotiwa ESPJ wa dola zaidi ya milioni 100. Mradi huu kimsingi unajaribu kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji katika vyuo vyote vinavyotoa elimu ya ufundi katika katika ngazi zote. Kwa hiyo, nimhakikishie tu kwamba ni kweli tunatambua umuhimu na ndiyo maana tunachukua hatua mbalimbali.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved