Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Masoud Abdalla Salim

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Mtambile

Primary Question

MHE. MASOUD A. SALIM aliuliza:- Kwa mujibu wa Ibara ya 141(2) ya Katiba ya Nchi, Deni la Taifa maana yake ni deni lenyewe, faida inayolipwa juu ya deni hilo, fedha zilizowekwa akiba kwa ajili ya kulipa deni hilo polepole na gharama zote zinazoambatana na deni hilo:- a) Je, Deni la Taifa hadi swali hili linajibiwa ni kiasi gani? b) Je, mchanganuo wa fedha zilizowekwa akiba kwa ajili ya kulipa deni hilo ukoje?

Supplementary Question 1

MHE. MASOUD A. SALIM: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwanza nionyeshe masikitiko yangu na mkanganyiko wa majibu ya taarifa zao mbalimbali za hali ya uchumi pamoja na utaalam wao wakitoa shule hapa Bungeni.
Mheshimiwa Spika, swali langu la kwanza, Deni la Taifa linaongezeka na mnaendelea kukopa madeni ya masharti ya kibiashara ambayo yanapelekea sisi Watanzania kupata matatizo makubwa wakati mkiandaa mazingira ya kutaka kulipa deni hilo nje au kama inavyotakiwa. Ukiangalia taarifa nyingine zinaeleza kwamba bado mna mpango wa kukopa Sh.4,840,000,000 kwa ajili ya kulipa Deni hilo la Taifa. Je, kwa hali hii ya uchumi ilivyo na mkakati huo wa kulipa Deni la Taifa mtahimili kweli au mnataka mnataka nchi iendelee kufilisika?
Mheshimiwa Spika, swali la pili ni kwamba Deni la Taifa halijafanyiwa uhakiki (credit rating) ili nchi yetu iweze kujiridhisha kwamba Serikali inakopesheka au haikopesheki. Naomba atuambie ni lini mkakati huo ufanyika haraka ili nchi yetu ifanyiwe credit rating hali iwe nzuri kama ambavyo inavyoendelea katika nchi nyingine?

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali ya Mheshimiwa Masoud Abdallah, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza kuhusu mkakati wa kulipa na kama deni letu ni stahimilivu, naomba nimwambie, kwanza Serikali yetu haijawahi ku-default hata mwezi mmoja katika kulipa madeni ambayo yameiva kwenye taasisi zote ambazo tumekopa. Ndiyo maana bado Taifa letu limeendelea kuaminiwa na taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa na tunaendelea kukopa kwa uangalifu wa hali ya juu. Tunapokopa tunahakikisha mikopo yote tunayoikopa tunapeleka katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi, ambapo tutaendelea kunyanyua uchumi wa Taifa letu na hasa tunapotelekeza azimio hili la Mheshimiwa Rais wetu la Tanzania ya Viwanda ambapo mpaka mwaka 2025 kwa uchumi wetu unavyokuwa tuna uhakika Taifa letu litakuwa ni Taifa la pato la uchumi wa kati. Napenda kuliambia Bunge lako Tukufu kwamba, kwa viashiria vyote kuhusu ukopaji na kulipa bado Taifa letu deni lake ni himilivu.
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusu credit rating, kama nilivyosema wakati tuna-conclude bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwamba mkataba ule upo ndani ya Ofisi ya AG na anaendelea kuufanyia rating ya mwisho. Tuna uhakika ndani ya mwaka ujao wa fedha Taifa letu litafanyiwa credit rating ili kujua sawasawa na mataifa yote duniani yaweze kufahamu kwamba Tanzania ni Taifa makini linaloaminiwa kiuchumi ndani na nje ya Taifa letu.

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MASOUD A. SALIM aliuliza:- Kwa mujibu wa Ibara ya 141(2) ya Katiba ya Nchi, Deni la Taifa maana yake ni deni lenyewe, faida inayolipwa juu ya deni hilo, fedha zilizowekwa akiba kwa ajili ya kulipa deni hilo polepole na gharama zote zinazoambatana na deni hilo:- a) Je, Deni la Taifa hadi swali hili linajibiwa ni kiasi gani? b) Je, mchanganuo wa fedha zilizowekwa akiba kwa ajili ya kulipa deni hilo ukoje?

Supplementary Question 2

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Swali langu linamuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha, je, ni lini Bunge pamoja na Wizara ya Fedha wataleta Muswada mpya wa kuweza kuidhibiti Serikali kukopa madeni kwa maana imeonekana tuna madeni makubwa na Serikali inakopa bila ya sisi Wabunge kufahamu?

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali moja la Mheshimiwa Sophia Mwakagenda, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali yetu ya Awamu ya Tano, kama ambavyo nimekuwa nikiliambia Bunge lako Tukufu tunafuata sheria, Katiba na taratibu zote za Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuhusu ukopaji Serikali yetu imeendelea kusimamia Deni la Taifa kwa kuzingatia Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, Sura 134. Hakuna hata siku moja ambapo Serikali yetu imekopa bila Bunge lako Tukufu kujulishwa na kupitisha. Huwa tunaleta tunavyoleta bajeti ya Serikali tunataraji kukopa kiasi gani, Bunge lako linaturuhusu na tunakwenda kukopa kile tulichoruhusiwa na Bunge lako Tukufu.

Name

Frank George Mwakajoka

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Tunduma

Primary Question

MHE. MASOUD A. SALIM aliuliza:- Kwa mujibu wa Ibara ya 141(2) ya Katiba ya Nchi, Deni la Taifa maana yake ni deni lenyewe, faida inayolipwa juu ya deni hilo, fedha zilizowekwa akiba kwa ajili ya kulipa deni hilo polepole na gharama zote zinazoambatana na deni hilo:- a) Je, Deni la Taifa hadi swali hili linajibiwa ni kiasi gani? b) Je, mchanganuo wa fedha zilizowekwa akiba kwa ajili ya kulipa deni hilo ukoje?

Supplementary Question 3

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kumekuwa na mkanganyiko mkubwa sana katika Deni hili la Taifa, Wabunge wamekuwa wakihoji sana kwamba deni limekuwa kubwa na wanahoji pia kwamba Serikali imekuwa ikikopa fedha na kulipia kwenye madeni ambayo tumekopa katika maeneo mengine. Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kuleta sheria ndani ya Bunge ili fedha yoyote inayokopwa na Serikali itakiwe kuidhinishwa ndani ya Bunge kwamba sasa Serikali ikope? Siyo Serikali inakopa tu halafu baadaye kunakuwa na hoja ambazo zinaleta mkanganyiko ndani Bunge hili na kwa Watanzania pia wanashindwa kujua fedha hizi zimefanya kazi gani. Ahsante.

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali moja la Mheshimiwa Frank, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kama nilivyomjibu Mheshimiwa Sophia Mwakagenda, Serikali hukopa baada ya Bunge lako Tukufu kupitisha kiwango kilichoombwa na Serikali kuhusu ukopaji huo na nimetaja sheria inayosimamia haya yote tunayoyatenda. Napenda kuliambia Bunge lako Tukufu kwamba katika kipindi ambacho Serikali yetu ilitakiwa kupongezwa ni kipindi cha Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa sababu tumeimarisha makusanyo ya mapato yetu ya ndani na tunalipa deni letu kupitia makusanyo ya mapato yetu ya ndani.