Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Willy Qulwi Qambalo
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Karatu
Primary Question
MHE. QAMBALO W. QULWI aliuliza:- Matukio ya Wanyamapori kutoka nje ya Hifadhi ya Ngorongoro kwenda katika vijiji vinavyopakana na hifadhi hiyo Wilayani Karatu na kuharibu mazao ya wananchi na kujeruhi watu yamekuwa yakijirudia mara kwa mara:- • Je, ni nini mkakati wa Serikali kuwadhibiti wanyama hao ili wabaki katika maeneo waliyotengewa; • Fidia/Kifuta jasho kinachotolewa pindi wanyama wanapofanya uharibifu ni kidogo sana na imepitwa na wakati. Je, ni lini Serikali italeta marekebisho ya kifuta jasho, ili kuendana na mazingira ya sasa?
Supplementary Question 1
MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali madogo ya nyongeza. Pamoja na kuwa na doria za pamoja kati ya halmashauri na hifadhi hizo na pamoja na kuwa na hivyo vituo vilivyotajwa bado kasi ya wanyama waharibifu na wakali kutoka ndani ya hifadhi na kwenda nje kwenye makazi ya wananchi, imeendelea kuwa kubwa mno.
Mheshimiwa Spika, changamoto kubwa ambayo tunayo kwenye Halmashauri zetu ni Halmashauri hazina usafiri kwa ajili ya kuwafukuza wanyama hao, Halmashauri hazina silaha stahiki kwa ajili ya wanyama hao, lakini pia, bajeti ndogo ambazo Halmashauri tunazo, pia, uchache wa watumishi wa sekta hiyo ya wanyamapori.
Mheshimiwa Spika, hapa imesemwa kuna magari mawili yamenunuliwa kwa ajili hiyo. Magari hayo mawili naamini yako Ngorongoro hayako Karatu huku ambako tatizo lilipo. Sasa Mheshimiwa Waziri anaweza akaongea na watu wake wa Ngorongoro ili angalau gari moja liwekwe Halmashauri, wale Maofisa wa Halmashauri pindi tatizo linapotokea waweze kwenda kushughulika?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, fedha hizi za kifuta jasho au kifuta machozi, pamoja na kwamba, ni ndogo sana lakini pia, zinachelewa sana kuwafikia...
Mheshimiwa Spika, swali; kwa nini fedha hizi zisilipwe kwenye hifadhi husika badala ya mlolongo ambao sasa hivi zinalipwa kutoka Wizarani? Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. (Makofi)
Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa kumekuwa na changamoto hizi za kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu katika maeneo mengi. Changamoto ziko katika upande wa usafiri, watumishi, pamoja na vifaa vile vinavyotakiwa kutumika katika kupambana na hao wanyamapori.
Mheshimiwa Spika, sasa niombe kusema tu kwamba, kama nilivyosema kwenye swali la msingi, magari mawili yameshanunuliwa na tayari kweli yako pale. jitihada ambazo tutafanya ni kulingana na jinsi ambavyo amependekeza Mheshimiwa Mbunge, kuhakikisha angalau gari moja linakuwepo katika maeneo yale kusudi pale linapotokea tukio basi gari hilo liweze kusaidia katika juhudi hizo za kupambana na wanyama wakali.
Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili, kuhusiana na fedha za kifuta jasho na kifuta machozi kwamba, ziwe zinatolewa na hifadhi inayohusika, ni suala ambalo labda tutaliangalia wakati tunapitia upya hizi sheria ambazo tutaona kama kweli, inafaa. Kwa hivi sasa ilivyo tuna mfuko maalum ambao unatumika kwa ajili ya kifuta jasho na kifuta machozi.
Mheshimiwa Spika, huu mfuko bado unakabiliwa na changamoto ya kuwa na fedha za kutosha. Kwa hiyo, katika pendekezo analolileta nafikiri tutaliangalia, tutaona kama linafaa, tunaweza tukalichukua. (Makofi)
Name
Cecilia Daniel Paresso
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. QAMBALO W. QULWI aliuliza:- Matukio ya Wanyamapori kutoka nje ya Hifadhi ya Ngorongoro kwenda katika vijiji vinavyopakana na hifadhi hiyo Wilayani Karatu na kuharibu mazao ya wananchi na kujeruhi watu yamekuwa yakijirudia mara kwa mara:- • Je, ni nini mkakati wa Serikali kuwadhibiti wanyama hao ili wabaki katika maeneo waliyotengewa; • Fidia/Kifuta jasho kinachotolewa pindi wanyama wanapofanya uharibifu ni kidogo sana na imepitwa na wakati. Je, ni lini Serikali italeta marekebisho ya kifuta jasho, ili kuendana na mazingira ya sasa?
Supplementary Question 2
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Changamoto ambazo zinakabili vijiji hapa nchini vinavyopakana na hifadhi za wanyama zimekuwa ni changamoto za muda mrefu kwamba, wanyama wanaingia na kuharibu mazao na kuuwa watu, lakini ukiangalia nchi mbalimbali zilizoendelea duniani wanaweka electrical fence, ili kudhibiti moja kwa moja tatizo hili. Je, Serikali kwa nini isianze kwa awamu kutekeleza na kuweka hizo electrical fence, ili angalau kukomesha kabisa tatizo hili? (Makofi)
Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Cecilia Paresso, dada yangu ambaye amekuwa akifuatilia kwa karibu sana matukio mbalimbali na amekuwa alifanya kazi nzuri sana, hongera sana.
Mheshimiwa Spika, sasa kuhusu electrical fence kuwekwa katika hifadhi zetu zote ni suala zuri, lakini uwezo wa kifedha ndiyo changamoto. Ukiangalia ukubwa wa hifadhi tulizonazo kwamba, zote tutaweka electrical fence kwa kweli, inaweza ikachukua muda mrefu sana. Sitaki kutoa commitment ya Serikali, lakini tutaendelea kulifanyia kazi ili tuone kwamba, kama litawezekana, kama pale ambapo bajeti itaruhusu basi tunaweza kulitekeleza.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved