Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Maftaha Abdallah Nachuma

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Mtwara Mjini

Primary Question

MHE. MAFTAHA A. NACHUMA aliuliza:- Serikali imeanzisha utaratibu wa kutoa elimu bure na kuanza kutekeleza utaratibu huo kwa kupeleka fedha shuleni kidogo kidogo kulingana na idadi ya wanafunzi husika tangu Oktoba 25, 2015:- (a) Je, Serikali inafahamu kwamba shule nyingi za msingi na za sekondari nchini zikiwemo za Mtwara Mjini zilikuwa na madeni mengi ya wazabuni na steshenari? (b) Je, Serikali inaweza kueleza kuwa madeni hayo yatalipwa kwa utaratibu upi ikiwa fedha zinazotolewa ni kidogo kwa uwiano wa mwezi kwa mwaka husika?

Supplementary Question 1

MHE. MAFTAHA A. NACHUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa sababu Serikali imeweza kutambua angalau kwamba kuna shilingi milioni 92.4 ambazo Manispaa ya Mtwara Mikindani inadaiwa, kwa maana ya shule za msingi na shule za sekondari. Naomba kuuliza maswali yafuatayo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, Shule ya Sekondari Sabasaba, Raha Leo, Chikongola na Shule zote za Msingi za Manispaa ya Mtwara Mikindani zinadaiwa hizi stationery kabla Serikali haijaanza utaratibu wa kupeleka elimu bure. Siku za nyuma ilikuwa michango inakusanywa kupitia kwa wazazi then zinalipwa stationery hizi ambazo zinatumika katika shule za msingi na sekondari. Ni lini Serikali italeta hizi shilingi bilioni 92.4 kwa ajili ya kulipa kwenye hizi shule ambazo zinadaiwa pale Mtwara Mjini? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari na Mwalimu Mkuu wa Shule za Msingi ndiyo wanaobeba haya madeni kama yao, ni declare tu interest nilikuwa Mkuu wa Shule, nafahamu kila Mkuu wa Shule anavyotembea anadaiwa yeye. Je, Serikali inawasaidiaje hawa Wakuu wa Shule za Sekondari na Walimu wa Shule za Msingi ili haya madeni yasionekane kama ni ya kwao yawe ni madeni ya Serikali na Serikali iweze kulipa kwa wakati? Ahsante (Makofi)

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Nachuma, Mbunge wa Mtwara Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza tumekiri kwamba Serikali kweli inadaiwa madeni hayo lakini utaratibu wake bado una mchakato ambapo tunahitaji kuyaangalia kwa undani zaidi madeni hayo. Ndiyo maana tumesema kwanza kuanzia Mwalimu Mkuu ajiridhishe na hayo madeni aandike barua kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kwamba nimeridhika kwamba madeni haya ni halali. Mkurugenzi wa Halmashauri alete tena kwetu tuyaangalie tena baadaye tutapeleka Wizara ya Fedha madeni ambayo tulishajiridhasha tena kwa mara nyingine sisi kwamba hayo ni halali halafu Serikali itaweka utaratibu wake vizuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali la pili kwamba tunawasaidiaje Wakuu wa Shule, wao wenyewe hasa wale waliokuwepo na Mheshimiwa Nachuma ulikuwepo na wewe umezalisha kumbe hayo madeni. Sasa wewe utakuwa shahidi mzuri vilevile katika kutuhakikishia kwamba madeni hayo ni halali. Kweli kama waajiriwa wetu Walimu Wakuu tumewakabidhi dhamana kubwa kwanza hatutaki waendelee kuzalisha madeni mengine kwa sababu sasa hivi tunapeleka fedha. Atakayezalisha deni lolote kuanzia sasa hivi itakuwa ni wajibu wake kulilipa kwa sababu tunapeleka hela sasa hivi. Kwa hiyo, kwa yale ya zamani tunaandaa huo mchakato kama nilivyokueleza katika swali la kwanza ili kusudi tuweze kuwaondolea huo mzigo wa madai.

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Primary Question

MHE. MAFTAHA A. NACHUMA aliuliza:- Serikali imeanzisha utaratibu wa kutoa elimu bure na kuanza kutekeleza utaratibu huo kwa kupeleka fedha shuleni kidogo kidogo kulingana na idadi ya wanafunzi husika tangu Oktoba 25, 2015:- (a) Je, Serikali inafahamu kwamba shule nyingi za msingi na za sekondari nchini zikiwemo za Mtwara Mjini zilikuwa na madeni mengi ya wazabuni na steshenari? (b) Je, Serikali inaweza kueleza kuwa madeni hayo yatalipwa kwa utaratibu upi ikiwa fedha zinazotolewa ni kidogo kwa uwiano wa mwezi kwa mwaka husika?

Supplementary Question 2

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa kuwa Serikali inatoa elimu ya bure kwa ngazi ya shule ya msingi na kwa kuwa wanafunzi walewale ambao wametoka shule ya msingi wanaenaenda sekondari kwa maana ya Form I - Form IV na wanafunzi haohao wanafaulu kwenda high school. Kwa sababu hao watoto walikuwa na mazoea ya kutokulipa ada, sasa wanahangaika mitaani kwa kukosa ada ya kwenda Form V. Je, nini kauli ya Serikali kuwasaidia watoto hawa ambao walipata msaada kutoka shule ya msingi wamefanikiwa kwenda sekondari na sasa wamefaulu kwenda high school na hawana uwezo wa kulipa ada? Ahsante.

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mwita Waitara, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba maoni kama hayo tumekuwa tukiyapata Serikalini siyo kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge peke yao bali hata kutoka kwa wananchi na NGOs mbalimbali. Hata hivyo niseme kwamba Ilani ya Uchaguzi ya CCM imeelekeza kwamba Serikali iandae utaratibu wa kutoa elimu msingi bila malipo ambayo ni kuanzia shule ya msingi mpaka Form IV. Kadri uwezo wa Serikali utakavyokuwa unavyoendelea kuwa mzuri zaidi inawezekana tukachukua ile Form V na VI na mambo yakiwa mazuri zaidi, Serikali ikavyojizatiti ikawa stable zaidi inawezekana tukatoa elimu bure mpaka chuo kikuu.

Name

Abdallah Dadi Chikota

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyamba

Primary Question

MHE. MAFTAHA A. NACHUMA aliuliza:- Serikali imeanzisha utaratibu wa kutoa elimu bure na kuanza kutekeleza utaratibu huo kwa kupeleka fedha shuleni kidogo kidogo kulingana na idadi ya wanafunzi husika tangu Oktoba 25, 2015:- (a) Je, Serikali inafahamu kwamba shule nyingi za msingi na za sekondari nchini zikiwemo za Mtwara Mjini zilikuwa na madeni mengi ya wazabuni na steshenari? (b) Je, Serikali inaweza kueleza kuwa madeni hayo yatalipwa kwa utaratibu upi ikiwa fedha zinazotolewa ni kidogo kwa uwiano wa mwezi kwa mwaka husika?

Supplementary Question 3

MHE. ABDALLAH D.CHIKOTA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa siku za nyuma Serikali ilijenga Vituo vingi vya Walimu (TRC) na kwa kuwa sasa hivi havitumiki kwa kukosa fedha, je, Serikali ina mpango gani wa kutumia sehemu ya fedha za elimu bure kupeleka kwenye Vituo vya Walimu ili ziendeshe semina kwa walimu hao katika maeneo yao?

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Abdallah Chikota kwa jinsi ambavyo anasimamia maendeleo kwenye Jimbo lake la Nanyamba na Mkoa wa Mtwara kwa ujumla na hata kulisaidia Bunge zima na Wizara yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi napenda nilichukue hili kama sehemu muhimu sana ya mchango wa mawazo mazuri na maoni Serikalini kwa ajili ya kulifanyia kazi. Ahsante.

Name

Omary Ahmad Badwel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bahi

Primary Question

MHE. MAFTAHA A. NACHUMA aliuliza:- Serikali imeanzisha utaratibu wa kutoa elimu bure na kuanza kutekeleza utaratibu huo kwa kupeleka fedha shuleni kidogo kidogo kulingana na idadi ya wanafunzi husika tangu Oktoba 25, 2015:- (a) Je, Serikali inafahamu kwamba shule nyingi za msingi na za sekondari nchini zikiwemo za Mtwara Mjini zilikuwa na madeni mengi ya wazabuni na steshenari? (b) Je, Serikali inaweza kueleza kuwa madeni hayo yatalipwa kwa utaratibu upi ikiwa fedha zinazotolewa ni kidogo kwa uwiano wa mwezi kwa mwaka husika?

Supplementary Question 4

MHE. OMARY A. BADWEL: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa lengo la Serikali kutoa fedha hizi katika shule za msingi ni kusaidia uboreshaji wa elimu hiyo na sasa ni takribani zaidi ya miaka miwili fedha hizi zimekuwa zikienda katika shule zetu za msingi na sekondari. Je, sasa Serikali katika utekelezaji wa jukumu hili imepata changamoto gani za matumizi sahihi na kuondoa ubadhirifu katika fedha hizi? Kama zipo changamoto hizo wamechukua hatua gani kutatua na kupunguza changamoto hizo?

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Omary Badwel, Mbunge wa Bahi, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama alivyosema kwamba sasa hivi tuna uzoefu wa miaka miwili katika kugharamia elimu msingi bila malipo. Napenda kuchukua nafasi hii kwa niaba ya Waziri wangu na Serikali kuwasifu sana wasimamizi wote wa elimu kuanzia Maafisa Elimu katika ngazi ya mkoa, wilaya na halmashauri na Wakaguzi wa Ubora na wasimamizi wa elimu katika ngazi ya kata, Maafisa Elimu wa Kata na Walimu Wakuu wa Shule za Msingi wamejitahidi sana kusimamia vizuri fedha hizi kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali. Maeneo machache sana ambayo yamekuwa na matatizo hatua zimechukuliwa na wengine wameshtakiwa kupitia Tume ya Utumishi wa Walimu na wachache sana ambao wameweza kuchukuliwa hatua. Siwezi kuwataja hapa kwa sababu idadi kamili sina lakini ni wachache sana ambao wamechukuliwa hatua. Kwa ujumla kazi ambayo sasa hivi inaendelea nchi nzima ni nzuri sana na wasimamizi wote wa sekta ya elimu wanastahili pongezi.

Name

Mary Pius Chatanda

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Korogwe Mjini

Primary Question

MHE. MAFTAHA A. NACHUMA aliuliza:- Serikali imeanzisha utaratibu wa kutoa elimu bure na kuanza kutekeleza utaratibu huo kwa kupeleka fedha shuleni kidogo kidogo kulingana na idadi ya wanafunzi husika tangu Oktoba 25, 2015:- (a) Je, Serikali inafahamu kwamba shule nyingi za msingi na za sekondari nchini zikiwemo za Mtwara Mjini zilikuwa na madeni mengi ya wazabuni na steshenari? (b) Je, Serikali inaweza kueleza kuwa madeni hayo yatalipwa kwa utaratibu upi ikiwa fedha zinazotolewa ni kidogo kwa uwiano wa mwezi kwa mwaka husika?

Supplementary Question 5

MHE. MARY P. CHATANDA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Kwa kuwa elimu ya msingi ni kuanzia elimu ya awali kwa maana chekechea. Kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya kupeleka fedha kwa kila kichwa cha mtoto kwenye elimu ya msingi, je, haioni sasa ni wakati muafaka wa kutoa fedha hata kwenye hii elimu kwa hawa watoto wa shule za awali ili kusudi ziweze kusaidia katika uendeshaji wa madarasa haya ya awali?

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mary Chatanda, Mbunge wa Korogwe Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumhakikishia kwamba elimu msingi bila malipo inaanzia madarasa ya awali ambayo ni sehemu ya shule za msingi na shule za sekondari hadi kidato cha nne. Tunapopeleka fedha kwenye kila shule mgawanyo wake umeainisha wanafunzi wote kuanzia madarasa ya awali mpaka la saba, kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha nne. Kwa hiyo, hakuna mtoto anayeachwa katika elimu msingi bila malipo kuanzia madarasa ya awali. Ahsante sana.