Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Khadija Nassir Ali
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. KHADIJA NASSIR ALI aliuliza:- Serikali imekuwa ikijitahidi kuvisimamia na kuviwezesha viwanda vyetu vya ndani lakini cha kusikitisha ni kwamba Serikali imeshindwa kusimamia bidhaa zetu ndani ya soko hili huria. Mathalani, bidhaa za viuadudu zinazozalishwa na kiwanda kilichopo Kibaha hazipo sokoni na wananchi hawana uelewa nazo:- Je, Serikali haioni kwamba kuendelea kuweka fedha kwenye viwanda vyetu bila ya kuwa na mikakati mizuri ya kibiashara ni kuendelea kutumia vibaya fedha za walipa kodi?
Supplementary Question 1
MHE. KHADIJA NASSIR ALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru namshukuru pia Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake. Nina maswali mawili ya nyongeza. Taarifa ya Mkaguzi Mkuu inaeleza kwamba kati ya lita 92,000 ya dawa hizo zilizosambazwa kwenye mikoa 26 ya Tanzania Bara ni lita 25,000 tu ndiyo ambazo zimeweza kutumika mpaka sasa. Ukizingatia dawa hizi zina life span, inawezekana kama hazijaharibika, sasa zinakaribia kuharibika. Serikali inatoa maelezo gani juu ya upungufu huo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, kwa kuwa dawa hizi zilisambazwa kwa mkopo wenye thamani ya shilingi bilioni 3.1 na makubaliano yalikuwa kwamba Halmashauri husika ziweze kulipa fedha hizi, Serikali ina
mkakati gani kusimamia fedha hizi ili ziweze kulipwa? Ahsante?
Name
Eng. Stella Martin Manyanya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nyasa
Answer
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Ni kwamba kimsingi dawa hizi ni muhimu sana na zinaua hasa katika maeneo yale ya mazalia. Sasa kama kuna Halmashauri zimechukua dawa hizo na zikaacha kupeleka kwenye maeneo hayo ya mazalia ya mbu kwa kweli wanatenda kosa kubwa kwa sababu wanawanyima wananchi haki yao ya kupona kutokana na kutokomeza viluwiluwi vya Malaria. Nawaomba wafanye hivyo mapema iwezekanavyo na wajue kwamba kufanya hivyo ni kurudisha nyuma jitihada za Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kuhusiana na madeni, ni kweli kabisa Halmashauri nyingi hazijaweza kulipa madeni waliyochukua dawa hizo. Kwa hiyo, nizitake pia Halmashauri kuhakikisha kwamba wanalipa madeni yao na kuyapa kipaumbele iwezekanavyo kuhakikisha kwamba wanalipa ili kutelekeza azma ya Serikali ya kukifanya kiwanda hicho kuwa endelevu.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved