Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Zuberi Mohamedi Kuchauka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Liwale
Primary Question
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza:- Msitu wa Nyera – Kipelele ni miongoni mwa misitu ya asili iliyopo Wilaya ya Liwale. Serikali imekuwa ikiandaa taratibu za uvunaji wa mazao ya msitu huo. (a) Je, taratibu hizo zitakamilika lini? (b) Je, Serikali imepata manufaa gani kutokana na uhifadhi wa msitu huo?
Supplementary Question 1
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri kutokana na swali hili. Kwa sababu sasa Harvesting Plan imekamilika ina maana sasa Serikali inaenda kuanza kupata mapato kutokana na msitu huo. Hata hivyo, kama ilivyo watu wa baharini au ziwani, uchumi wao mwingi unategemea mali ya bahari na mali ya ziwa. Vilevile sisi tulio kwenye misitu uchumi wetu mkubwa unategemea mazao ya misitu. Sasa kwa nini Serikali mpaka leo hii ile cess haijapata kuongezwa kutoka asilimia tano tunayoipata kutokana na uvunaji huu wa misitu, angalau ifike asilimia 10 ili kuweza kuinua kipato cha Halmashauri tunazozunguka?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, TFS wamekuwa na tabia ya kutotoa ile responsibility kwa vijiji vyetu yaani ile incentive. Sio hivyo tu kuna mazao ambayo yamevunwa na wavunaji haramu ambayo yapo kwenye Halmashauri zetu kwa muda mrefu yanaendelea kuharibika. Je, Serikali haioni sasa inaweza kutoa kwenye Halmashauri husika yale mazao ambayo yamevunwa kwa haramu ili yaweze kunufaisha kwenye vijiji vyetu, kwa mfano mazao ya mbao, yanaweza kutusaidia kutengeneza furniture au viti, meza na madawati kwa ajili ya shule zetu na hospitali zetu?
Name
Constantine John Kanyasu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Geita Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, asilimia tano ya cess ambayo TFS wamekuwa wakitoa kwenye Halmashauri, iko kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982 na sisi kama Wizara hatuwezi kuibadilisha na hatuwezi kuikiuka. Kwa hiyo Mheshimiwa Mbunge kama anataka ibadilike anaweza kuanzisha mchakato huo, lakini kwa sasa maelekezo yetu ni kutoa asilimia tano.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, ni kweli kwamba maeneo ya Liwale kuna mbao nyingi ambazo zilikamatwa wakati wa Operation Tokomeza, na mbao hizo bado kesi zake ziko Mahakamani. Hata hivyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, mara uvunaji huu niliosema utakapoanza, tutawaelekeza TFS kuhakikisha kwamba wanatoa misaada kwenye shule zote ambazo ziko jirani na maeneo ya uvunaji.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved