Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Tauhida Cassian Gallos Nyimbo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TAUHIDA CASSIAN GALLOS NYIMBO aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani juu ya raia wa kigeni wanaopewa vibali vya kuja kufanya kazi hapa nchini kwa muda na kuwazalisha watoto na wadogo zetu na inapofika muda wa kuondoka huwakimbia na kuwaacha watoto hao wakiishi maisha yao yote bila baba kitu ambacho huwasababishia unyonge katika maisha yao?

Supplementary Question 1

MHE. TAUHIDA CASSIAN GALLOS NYIMBO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa fursa hii ya kuuliza maswali mawili. Ningependa kufahamu njia gani zinazotumika katika kutoa elimu hiyo hususan vijijini?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili kwa kuwa Mkuu wa Mkoa amekuwa mdau mkubwa wa kuwapigania watoto wanaoachwa na wazazi wao wa kiume, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa kuja na sheria za kuwabana wanaoacha watoto hususan wakiwemo na raia wa kigeni.

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza kwa pamoja ya Mheshimiwa Tauhida kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa tunayo sheria ambayo inaharamisha matukio ambayo yanahusisha mtu yeyote kutelekeza mtoto ama kutotoa matunzo na sheria hiyo si nyingine ni Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 kifungu cha 166, kwa hiyo sheria tunayo tayari. Niwaombe akinamama wote ambao wameathirika na jambo hili kwa kuwa ni la jinai, waende kwenye vituo vya polisi vilivyo karibu wafungue kesi hizi ili Serikali tutumie sheria nyingine zozote tulizonazo za kuwarejesha nchini wajibu mashtaka.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo zoezi alilolifanya Mheshimiwa Makonda Mkuu wa Mkoa ambalo Mheshimiwa Mbunge ame-refer ni zoezi ambalo lilionyesha dhahiri kwamba sio wageni tu wanaotelekeza watoto isipokuwa hata Watanzania wanatelekeza watoto na tulishuhudia wengine humu ndani sura za watoto zikiwa zinawafanana.

Mheshimiwa Spika, nitoe wito kwa akinamama wa Tanzania, nawaomba mtumie kilicho ndani ya nchi, kilicho chenu kuliko kuanza kukimbilia kutumia raia wa kigeni ilhali hata humu ndani, rudini humu ndani kumenoga.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.