Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Richard Phillip Mbogo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nsimbo
Primary Question
MHE. RICHARD P. MBOGO aliuliza:- Mabadiliko ya Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa Sura 290 yameleta nafuu sana kwa wakulima, lakini wakati huo huo Halmashauri za Wilaya zenye wakulima wadogo zimeathirika kimapato na kusababisha kushindwa kutatua kero za wananchi kwa wakati. (a) Je, Serikali inaweza kuangalia upya suala la utaoji ruzuku za maendeleo? (b) Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imeathirika kwa kiwango kikubwa: Je, Serikali ipo tayari kuipatia ruzuku ili kutoa huduma za elimu na afya?
Supplementary Question 1
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi. Pamoja na majibu ya Serikali, tunajua ongezeko la mapato. Tuna Halmashauri 185 lakini zinatofautiana kati ya Halmashauri na Halmashauri. Kwa hiyo, pamoja na ongezeko la kibajeti, bado Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imeathirika na mabadiliko ya Sheria hii. Sasa je, Serikali iko tayari kuongeza ruzuku toka hii ambayo tumeipata ya shilingi milioni 250 ambapo tumeweza kumalizia maboma ya shule mbalimbali?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; tuna changamoto pia upande wa huduma za kiafya. Kata ya Itenka pamoja na Kata ya Ugara ziko mbali sana na upatikanaji wa huduma: Je, Serikali iko tayari kutupatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya katika Kata hizi mbili?
Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Serikali iko tayari kuendelea kukamilisha maboma ya afya na elimu na ndiyo maana Mwezi wa Pili tumepeleka fedha zaidi ya shilingi bilioni 29.9 katika Majimbo mbalimbali likiwepo na hili la Nsimbo kukamilisha maboma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika jibu langu la msingi nimesema, Serikali itaendelea kupeleka fedha ya ruzuku ya miradi ya maendeleo mbalimbali kadri ambavyo fedha itapatikana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili anaulizia kuwa na vituo vya afya. Ni nia njema ya Serikali kuendelea kuimarisha huduma za afya na tumefanya hivyo, vimejengwa vituo 352. Kwenye bajeti hii ambayo tunaendelea na mjadala kwenye Bunge lako Tukufu tunavyo vituo 52 vingine, hospitali 27, ukiongeza zile 67 zilizopo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimtie moyo Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaendelea kufanya kazi hii ya kutoa huduma ya afya kwa wananchi wake kadri ya upatikanaji wa fedha. Ahsante.
Name
Pauline Philipo Gekul
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Babati Mjini
Primary Question
MHE. RICHARD P. MBOGO aliuliza:- Mabadiliko ya Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa Sura 290 yameleta nafuu sana kwa wakulima, lakini wakati huo huo Halmashauri za Wilaya zenye wakulima wadogo zimeathirika kimapato na kusababisha kushindwa kutatua kero za wananchi kwa wakati. (a) Je, Serikali inaweza kuangalia upya suala la utaoji ruzuku za maendeleo? (b) Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imeathirika kwa kiwango kikubwa: Je, Serikali ipo tayari kuipatia ruzuku ili kutoa huduma za elimu na afya?
Supplementary Question 2
MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza. Pamoja na Halmashauri zetu kufanya vizuri, kuna baadhi ya vyanzo hawafanyi vizuri. Mfano, chanzo cha Kodi ya Ardhi, mwanzoni walikuwa wakikusanya wanapata retention ya 30 percent lakini sasa hawapati retention hiyo ambayo ilikuwa inawasaidia kujaza gari mafuta waweze kufuatilia wale ambao hawalipi Kodi ya Ardhi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nifahamu: Je, Serikali iko tayari kuangalia upya chanzo hili ili kisaidie kukusanya kodi hii ya ardhi kwa asilimia 100?
Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza nampongeza Mheshimiwa Gekul kwa kazi nzuri anayoifanya kule Babati kuwasemea watu wa Babati, lakini pili, naomba nilipokee suala hili kama sehemu ya changamoto, tuwasiliane na Halmashauri ya Babati Mjini, Wizara ya Ardhi na TAMISEMI tuone changamoto zilizopo tuweze kuziimarisha.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved