Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Juma Othman Hija
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tumbatu
Primary Question
MHE. JUMA OTHMAN HIJA aliuliza:- Thamani ya Shilingi ya Tanzania inaendelea kuporomoka kila siku, kuporomoka huko kunachangia kwa kiasi fulani ugumu wa maisha kwa wananchi wa kawaida katika kupanga mipango yao ya kimaisha:- Je, Serikali ina mkakati gani ya kudhibiti mporomoko huo?
Supplementary Question 1
MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri na ya kutosheleza kabisa, lakini nina swali moja dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni Serikali imekuwa na zoezi la kuyafungia maduka ya Bureau De Change nchi nzima. Je, zoezi hili ni miongoni mwa mikakati ya kuimarisha fedha yetu au ni kwa madhumuni gani?
Name
Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Kondoa
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali moja la Mheshimiwa Juma Othman Hija, Mbunge wa Tumbatu kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyouliza je, ulikuwa ni mkakati wa kuhakikisha thamani ya fedha yetu. Kama nilivyoeleza kwenye jibu langu la msingi moja ya kazi za benki kuu ni kuhakikisha kwamba thamani ya fedha yetu inakuwa imara na katika mikakati ya kuhakikisha hilo, ni kuhakikisha kunakuwa na usimamizi imara na madhubuti wa maduka yetu ya kubadilisha fedha na hilo ndilo lilikuwa lengo la zoezi lililofanyika.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved