Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Machano Othman Said

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. MACHANO OTHMAN SAID aliuliza:- (a) Je, ni Wizara ipi inayo wajibika kukusanya fedha za Viza na kusimamia utoaji wa Viza hizo? (b) Je, kuna mgao wowote kwenda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia uwanja wake wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume?

Supplementary Question 1

MHE. MACHANO OTHMAN SAID: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake, lakini pamoja na majibu hayo, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Kwa kuwa Wizara mbili zinahusika sana na makusanyo ya Viza katika nchi za nje kupitia Balozi zetu. Je, Wizara ya Mambo ya Ndani inakuwa inafanya nini katika kuhakikisha fedha hizo na zinawekwa katika vitabu vya Wizara gani?

Pili, katika mwaka wa fedha 2018/2019 wa bajeti, Viza kwa upande wa Zanzibar zimekusanywa kiasi gani kwa sababu tuna watalii zaidi ya 500,000 kwa mwaka. Je, ni kiasi gani cha fedha ambacho kimekusanywa kwa kupitia Zanzibar?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kuhusu hoja ya kwamba kuna Wizara mbili zinashughulikia nataka nimthibitishie tu kwamba baada ya Mheshimiwa Rais kuzindua utaratibu wa kuwa na mfumo wa e-visa ambayo inahusisha, tunapuzungumzia immigration inahusisha e-visa e-passport n.k. na sasa hivi nitoe taarifa hii hapo Bungeni kwamba mfumo huu umeshafungwa katika Balozi zetu nchi za nje. Kwa hiyo, sasa ile changamoto ambayo ilikuwepo mwanzo, haipo. Sasa hivi fedha yote tena inaingia katika mfumo na hivyo basi hiyo hoja ambayo Mheshimiwa ameuliza imeshapatiwa ufumbuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na takwimu naomba nimhakikishie Mheshimiwa Machano kwamba nitampatia hizo takwimu baadaye.