Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Silafu Jumbe Maufi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SILAFU J. MAUFI aliuliza:- Mkoa wa Rukwa umeanzishwa mwaka 1974 lakini hadi sasa hakuna viwanda vikubwa vilivyowekezwa na kuwekewa mikakati na Serikali na viwanda vilivyopo ni vya watu binafsi:- (a) Je, Serikali ina mikakati gani ya kujenga viwanda au kupeleka wawekezaji ambao watajenga viwanda vikubwa Mkoa wa Rukwa ili kutoa ajira kwa vijana? (b) Mazao yanayolimwa Mkoa wa Rukwa yanapewa bei kiholela na kufanya maisha ya wananchi kuwa magumu: Je, ni lini Serikali itaingia mkataba na viwanda vya uzalishaji?

Supplementary Question 1

MHE. SILAFU J. MAUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri, lakini bado napenda kufahamu kwamba, ikiwa mikoa na wilaya zimeweza kutanganza fursa ambazo zimo ndani ya mikoa husika, lakini bado mikoa ile ama wilaya zile zinasuasua katika kupata wawekezaji; Je, Serikali haioni umuhimu wa wao wenyewe kwenda kusukuma katika mikoa ile na wilaya zile kuweza kupata viwanda hivyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili la nyongeza, napenda kufahamu kwamba wanapewa muda upi wa utangazaji wa fursa na kama fursa haina majibu Serikali inachukuwa mkakati gani katika mkoa huo?

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Maufi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue nafasi hii kuupongeza sana Mkoa wa Rukwa umekuwa ukifanya makongamano mbalimbali ya kuhamasisha uwekezaji na makongamano hayo kwa kweli yamekuwa yakiza matunda. Kwa mfano, wameweza kuhamasisha na kupata kiwanda cha kusindika unga wa mahindi, Kiwanda cha Energy, vilevile wameweza kuhamasisha na mpaka kuwezesha mradi wa makaa ya mawe kuanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niseme tu kwamba Serikali hatuiachi mikoa peke yao isipokuwa mikoa yenyewe kwa sababu inazo fursa hizo kwa karibu zaidi inapohamasisha inaungana na Serikali Kuu kuona kwamba hawa wenye viwanda waweze kwenda kuwekeza huko. Sisi kwa kutumia Tantrade, TIC na Wizara kwa ujumla kwa kushirikiana na Wizara ya Uwekezaji tumekuwa tukiendelea kuhamasisha wenye viwanda au wawekezaji mbalimbali kwenda kwenye maeneo hayo.

Name

Goodluck Asaph Mlinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ulanga

Primary Question

MHE. SILAFU J. MAUFI aliuliza:- Mkoa wa Rukwa umeanzishwa mwaka 1974 lakini hadi sasa hakuna viwanda vikubwa vilivyowekezwa na kuwekewa mikakati na Serikali na viwanda vilivyopo ni vya watu binafsi:- (a) Je, Serikali ina mikakati gani ya kujenga viwanda au kupeleka wawekezaji ambao watajenga viwanda vikubwa Mkoa wa Rukwa ili kutoa ajira kwa vijana? (b) Mazao yanayolimwa Mkoa wa Rukwa yanapewa bei kiholela na kufanya maisha ya wananchi kuwa magumu: Je, ni lini Serikali itaingia mkataba na viwanda vya uzalishaji?

Supplementary Question 2

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa ambayo ilikuwa vinara wa kuwa na viwanda vingi na imekuwa ikitoa ajira nyingi sana kwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro enzi hizo za ujana wetu.

MWENYEKITI: Uliza swali.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, vilikuwepo viwanda vya maturubai, magunia, ngozi, mafuta ya kupikia, vipuli vya mashine, mazulia hata Ulanga tulikuwa na kiwanda cha pamba lakini baada ya ubinafsishaji viwanda vyote vikawa kushne, vikawa magofu ya kufugia mbuzi na Serikali imekuwa ikipiga mikwara mara kwa mara…

MWENYEKITI: Uliza swali Mheshimiwa.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Je, Serikali inatoa kauli gani sasa kwa magofu hayo ambayo yamegeuzwa na wawekezaji badala ya kufanywa kuwa viwanda?

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Goodluck, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kauli ya Serikali ni kwamba wale wote waliokuwa wamebinafsishiwa viwanda na hawajaweza kuviendeleza kama ambavyo mkataba wao ulikuwa na ambavyo Serikali ilitarajia, tunatarajia viwanda hivyo vitarejeshwa. Mpaka sasa Serikali imesharejesha viwanda 15 na tunaendelea na zoezi hilo ili hivi viwanda viweze kufanya kazi kwa tija iliyokusudiwa.

Name

Mary Pius Chatanda

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Korogwe Mjini

Primary Question

MHE. SILAFU J. MAUFI aliuliza:- Mkoa wa Rukwa umeanzishwa mwaka 1974 lakini hadi sasa hakuna viwanda vikubwa vilivyowekezwa na kuwekewa mikakati na Serikali na viwanda vilivyopo ni vya watu binafsi:- (a) Je, Serikali ina mikakati gani ya kujenga viwanda au kupeleka wawekezaji ambao watajenga viwanda vikubwa Mkoa wa Rukwa ili kutoa ajira kwa vijana? (b) Mazao yanayolimwa Mkoa wa Rukwa yanapewa bei kiholela na kufanya maisha ya wananchi kuwa magumu: Je, ni lini Serikali itaingia mkataba na viwanda vya uzalishaji?

Supplementary Question 3

MHE. MARY P. CHATANDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ili nami niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Korogwe Mji tulikuwa na kiwanda cha matunda na kama tunavyofahamu Mkoa wa Tanga una kilimo sana cha matunda. Kiwanda kile baada ya kubinafsishwa, yule mwekezaji ni miaka karibu 20 sasa kiwanda kile alishang’oa mashine zote na mabati yote yameshatolewa. Je, mtakuwa tayari sasa kutukabidhi eneo lile ili kusudi tuweze kuwawekea vijana shughuli za kufanya katika eneo lile?

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la Mheshimiwa Mary Chatanda, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi kiwanda hicho kinachozungumzwa nimekitembelea na kwa kweli hatuwezi kuendelea kukiita kiwanda na Mheshimiwa Waziri alishakitolea kauli ya kukifuta katika orodha ya viwanda. Kwa hiyo, kama ni eneo, naamini linaweza likatumika kwa Halmashauri inayohusika.

Name

Cecil David Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ndanda

Primary Question

MHE. SILAFU J. MAUFI aliuliza:- Mkoa wa Rukwa umeanzishwa mwaka 1974 lakini hadi sasa hakuna viwanda vikubwa vilivyowekezwa na kuwekewa mikakati na Serikali na viwanda vilivyopo ni vya watu binafsi:- (a) Je, Serikali ina mikakati gani ya kujenga viwanda au kupeleka wawekezaji ambao watajenga viwanda vikubwa Mkoa wa Rukwa ili kutoa ajira kwa vijana? (b) Mazao yanayolimwa Mkoa wa Rukwa yanapewa bei kiholela na kufanya maisha ya wananchi kuwa magumu: Je, ni lini Serikali itaingia mkataba na viwanda vya uzalishaji?

Supplementary Question 4

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Msingi wa swali langu uko kwenye swali namba 170, kipengele (b) kuhusiana na suala la bei ya mazao kwamba imekuwa ni holela.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda sasa Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara itueleze, kwa sababu watu wa Wizara ya Kilimo wanasema wao walishamaliza kazi ya kukusanya, je, korosho ghafi na korosho iliyobanguliwa mnaiuza kwa shilingi ngapi?

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mwambe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi baada ya Serikali kufanya uamuzi wenye hekima kabisa wa kununua korosho kwa hawa wananchi ili kuwapunguzia maumivu ya kuuza kwa bei mbaya, korosho iliyopo sasa hivi tunaendelea kuiuza na hatujapanga bei maalum, inategemeana na mteja anavyokuja na pale itapofikia sisi kuwa imelipa gharama zetu zile ambazo tulitumia. Kwa misingi hiyo, nikuombe Mheshimiwa Mwambe ukiwa pia ni mdau na mwananchi mwingine yeyote anayenisikia hata watu wa nje korosho ghafi zipo na zilizobanguliwa zaidi ya tani 391 zipo na ziko katika hali nzuri basi yeyote anayetaka kununua karibu sana aweze kuuziwa.

Name

Masoud Abdalla Salim

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Mtambile

Primary Question

MHE. SILAFU J. MAUFI aliuliza:- Mkoa wa Rukwa umeanzishwa mwaka 1974 lakini hadi sasa hakuna viwanda vikubwa vilivyowekezwa na kuwekewa mikakati na Serikali na viwanda vilivyopo ni vya watu binafsi:- (a) Je, Serikali ina mikakati gani ya kujenga viwanda au kupeleka wawekezaji ambao watajenga viwanda vikubwa Mkoa wa Rukwa ili kutoa ajira kwa vijana? (b) Mazao yanayolimwa Mkoa wa Rukwa yanapewa bei kiholela na kufanya maisha ya wananchi kuwa magumu: Je, ni lini Serikali itaingia mkataba na viwanda vya uzalishaji?

Supplementary Question 5

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kunipa nafasi ya kuuliza swali moja dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katika miaka ya 70 na 80 Serikali ilikopa kutoka Japan na Italia dola milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya korosho katika Mikoa ya Lindi na Mtwara. Wakati wa ubinafsishaji viwanda hivyo vilibinafsishwa lakini hadi leo viwanda hivyo havifanyi kazi. Mara nyingi Serikali imesema hapa Bungeni itakaa na wawekezaji kuona kwamba…

MWENYEKITI: Hebu uliza swali Mheshimiwa.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali linakuja, ni kwa nini Serikali imelidanganya Bunge mara kadhaa kwamba itakaa na wawekezaji ili waweze kusaidia viwanda hivi na wananchi wapate manufaa yanayohitajika?

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Masoud, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi katika viwanda hivyo vipo ambavyo vinafanya kazi vizuri na vimeajiri zaidi ya watu 750 kwa kimoja. Kwa mfano, kiwanda cha Tunduru, cha Korosho Afrika lakini pia Kiwanda cha Newala Micronics, hivyo vimeajiri watu 750 kila kimoja lakini pia Micronics pale Mtwara kimeajiri kama watu 350. Vilevile kuna Kiwanda cha Mtwara kinachohusika na korosho pia ambacho sasa hivi ndicho kinachosaidia kufungasha hizo korosho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiri kuna baadhi ya viwanda havikufanya vizuri, kwa mfano, Kiwanda cha Mtama na Kiwanda cha Nachingwea, hivyo tumeshavinyang’anya. Pia kuna Kiwanda cha Lindi Buko, nacho tumeshakinyang’anya na tumeshaanza kukifufua. Hiyo ndiyo hali halisi.