Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Ally Yusuf Suleiman

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Mgogoni

Primary Question

MHE. DKT. SULEIMAN ALLY YUSSUF aliuliza:- Ibara ya 130 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inataja kazi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, moja ya kazi zake ni kufanya uchunguzi juu ya mambo yanayohusu uvunjaji wa Haki za za Binadamu na ukiukwaji wa msingi ya utwala bora. (a) Je, kwa nini ripoti za tume hiyo haziwekwi wazi kwa Umma? (b) Je, Serikali haioni kuwa umefika wakati wa kujenga utamaduni wa ripoti hizo kujadiliwa Bungeni?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. SULEIMAN ALLY YUSSUF: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana jambo la kwanza nataka nimwambie Mheshimiwa Naibu Waziri nimerekebisha waliodhurumiwa katika haki za Binadamu. Na ningeweza kujibu sana lakini sio wakati wake. Maswali yangu mawili, kituo cha haki za binadamu LHRC Tanzania huwa kinaweka wazi matukio yote makubwa ambayo yanayotokea nchini yakiwemo utekwaji, uteswaji, upoteaji, upigwaji risasi, kuonyesha bastola hadharani….

MWENYEKITI: Uliza swali sasa.

MHE. DKT. SULEIMAN ALLY YUSSUF: Ubambikizwaji…

MWENYEKITI: Uliza swali sasa

MHE. DKT. SULEIMAN ALLY YUSSUF: Ripoti za Serikali hazibebi mambo mazito kama haya.

Swali la pili, nataka kujua ni challenge zipi ambazo serikali inazipata inapokwenda kutoa ripoti zake katika vikao vya kimataifa huku kukiwepo na ripoti mbadala za ndani zinazo kinzana na ripoti za Serikali?

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): Mheshimiwa
Mwenyekiti, ni kweli Legal Human Right Center mara nyingi hutoa ripoti yenyewe inavyoona kuwa mambo ya haki za binadamu yamekuwa yakiendelea nchini, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba sheria zetu zina ruhusu na inatoa uhuru wa maoni sio Legal Human Right Center hata watu binafsi mashirika mengine sio ya kiserikali kwa hiyo wanaongea mengi. Lakini katiba na sheria zetu zimetambua hasa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwamba ndio imepewa jukumu la kikatiba la kuhakikisha kwamba haki za binadamu zina heshimiwa na ndio imepewa fursa ya kusikiliza malalamiko mbalimbali. kwa hiyo, yoyote yule mwenye malalamiko na manunguniko kuhusiana na uvunjifu wa haki za binadamu pamoja na ufunjivu wa taratibu za utawala bora waweze upeleka kwenye Tume kama inavyotakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ni changamoto gani tunapata huko tunapoenda nje kuhusiana na haki ya haki za binadamu, naomba nimfahamishe Mheshimiwa Mbunge kwamba changamoto kubwa kuliko zote ni uposhwaji mkubwa sana unaofanywa na sio tu taasisi mbalimbali lakini vilevile mtu mmoja mmoja ikiwa na baadhi na wanasiasa. Lakini kama anavyofahamu hivi karibuni Serikali imeamua kuchukua hatua kuhakikisha kwamba kila upotoshwaji unaotolewa unajibiwa pale unapotolewa kwa sababu mara nyingi ni kwa ajili ya kuchafua sifa njema ya Taifa letu.