Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ally Abdulla Ally Saleh
Sex
Male
Party
CUF
Constituent
Malindi
Primary Question
MHE. ALLY SALEH ALLY aliuliza:- Moja ya misingi mikuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ni utawala bora, haki za binadamu na demokrasia sambamba na kukuza uchumi za Nchi sita Wanachama:- (a) Je, hilo linatimizwa kwa kiasi gani ndani ya Jumuiya na Wanachama? (b) Je, kuna mfumo gani wa kukosoana ndani ya Jumuiya katika eneo hilo?
Supplementary Question 1
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, base ya swali langu ni kwamba na-target Jumuiya, Nchi Wanachama na wananchi wanafaidikaje na hali hiyo. Sasa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ndio chanzo cha awali kabisa cha kupima utawala bora kwa upande wa haki ya kuchagua na kuchaguliwa, haki ya maoni na kujieleza kwa hapa njia ya kufanya kampeni, lakini pia ni kigezo cha kupata Serikali Shirikishi kadri inavyowezekana.
Je, kwa hali hii ya wagombeaji kutoka upande wa upinzani kukatwa kwa zaidi ya asilimia 90. Je, Tanzania haioni kwamba inakiuka matakwa hayo ya Afrika Mashariki?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili kwa matukio tunayoyaona hapa nchini madai ya haki za binadamu ambayo hata Human Right International Watch juzi imetutaja lakini pia kwamba ku-shrink kwa public space pia kuwanyima wananchi fursa ya kuona Bunge live, kuwaweka mashehe wa kiislamu kwa miaka saba ndani bila kuwafungulia shauri na pia kutokuwa na Tume Huru…
MWENYEKITI: Sasa Mheshimiwa Ally Saleh, swali unaongeza, unaongeza uliza mawili tu moja tayari, la pili malizia.
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Je, Serikali ya Tanzania haioni kwamba haikidhi vigezo vya kuwa na utawala bora na haki za binadamu? (Makofi)
Name
Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Songea Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza anasema je, Tanzania haikiuki viwango kwa mujibu wa Afrika Mashariki. Tanzania ni nchi ambayo inafuata misingi ya utawala bora, misingi ya haki ya binadamu kama ambavyo imeainishwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nyaraka nyingine za Kimataifa. Endapo kunatokea malalamiko yoyote tumesema bayana kupitia Afrika Mashariki, yeyote ambaye amekwazwa na lolote anaweza akaenda kulalamika kupitia Bunge la Afrika Mashariki pia kupitia Mahakama ya Afrika Mashariki na Serikali ya Tanzania ndio imeamua kuwa mwanachama ili kuwapa fursa wananchi wake kutoa malalamiko kwenye vyombo hivyo. Hicho ni kitendo cha wazi kabisa kwamba Serikali hii inaweza na inajali haki za binadamu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, amesema pia kuna malalamiko kuna Human Right International Watch; malalamiko yanatoka mengi sana, ni vizuri yachunguzwe, yanatoka wapi, yanaletwa na nani na kwa nia ipi na yakifika yashughulikiwe kwa mujibu wa muundo ambao unao. Hata hivyo, nimhakikishie Mheshimiwa Ally Saleh (Alberto), Mbunge wa Malindi kwamba Tanzania ni nchi ambayo inaheshimu sana haki za binadamu, demokrasia na utawala bora. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved