Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Desderius John Mipata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkasi Kusini

Primary Question

MHE. DESDERIUS J. MIPATA aliuliza:- Wananchi wa Kijiji cha Kasapa walikuwa na ombi la kuongezewa maeneo ya kilimo kutoka kwenye eneo la Hifadhi ya Kalambo TFS:- Je, Serikali imefikia hatua gani katika utekelezaji wa ombi hilo la wananchi wa Kijiji cha Kasapa?

Supplementary Question 1

MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana nina maswali mawili ya nyongeza. Kwanza nishukuru sana majibu mazuri ya Serikali, naomba tu utekelezaji uwe wa haraka kwa sababu msimu wa mvua karibu unafika. Katika operasheni zao mbalimbali, watu wa Maliasili wa Luafi Game Reserve wamekuwa wakiwafukuza wananchi usiku kwenye Vijiji vya King’ombe, Lundwe, Mlalambo, Kizumbi na Lupata: Je, utaratibu huo hauwezi kubadilika ili operesheni zao wafanye mchana ili sheria zifuate taratibu zake?

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Kigwangalla alipofanya ziara Wilayani kwetu, aliahidi kutoa bati katika Kijiji China katika ujenzi wao wa zahanati: Je, bati hizi zitatolewa lini? (Makofi)

Name

Dr. Hamisi Andrea Kigwangalla

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Vijijini

Answer

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Naomba nijibu hili la bati, la kwanza atajibu Mheshimiwa Naibu Waziri.

Mheshimiwa Spika, naomba niwasiliane na Mheshimiwa Mbunge baada ya Bunge hili kwisha ili tuweze kuona hatua stahiki za kuchukuliwa ili ahadi hiyo iweze kutekelezwa mara moja. (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, kwanza nimuhakikishie kwamba kama kuna Askari wetu wa Wanyamapori badala ya kufanya operation mchana anakwenda usiku kufungua nyumba za watu anafanya makosa, maelekezo ambayo ninayatoa hapa ni kwamba operation hizo zifanyike mchana na zisifanyike usiku kwa mujibu wa sheria.(Makofi)