Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Fakharia Shomar Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS aliuliza:- Askari wa Jeshi la Polisi Zanzibar (Ziwani) wanakabiliwa na matatizo makubwa ya makazi kama vile miundombinu ya maji, nyumba chakavu, uhaba wa vyoo na kuharibika kwa uzio uliokuwepo katika eneo hilo unaohatarisha usalama wao:- (a) Je, kuna mpango gani wa kufanyia matengenezo nyumba na vyoo kwa wakati huu? (b) Je, Uzio wa boma hilo la Ziwani utafanyiwa ukarabati?
Supplementary Question 1
MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Spika, ahsante. Sina budi kumshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa jawabu alilonipa ambalo ni zuri na linaridhisha na kaamua kusema ukweli wake hali halisi ya Kambi hiyo, lakini ni nana maswali mawili ya nyongeza:-
Kwa kuwa, uzio ambao ninaupigia kelele kila siku, sasa hivi wanataka waukarabati kufanya wa matofali na sasa bado upo wa waya, lakini hata hivyo wamejitahidi upande wa School ya Jang’ombe tayari wameufanyia ukarabati, ningeomba na upande wa Matarumbeta, upande wa kwa Alinatu, upande wa Kwahani kwa sababu hizo njia za panya zimekaa sehemu mbaya na watu bado wanazitumia kama vichaka au njia za kupitia wangelifanya kila mbinu na sehemu hizo wakafanyia ukarabati kabla hata kufanya ukarabati huo utakaozungushwa kwa matofali.
Swali la pili, kwa kuwa tayari amekubali kwamba nyumba za kambi hizo zote zimechakaa na kweli zimechakaa, maana zimejengwa kabla ya Mapinduzi ya 1964 na kwa kuwa nyumba hizo hasa zili wanazokaa Askari wa wa kawaida siyo Maofisa ambao ni kama mabanda nyumba hizo zimechakaa na haziridhishi kukaa binadamu ningeomba angalau wangeanza kuzifanyia ukarabati hizo ili Askari wetu wakaishi maisha bora.
Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. (Makofi)
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI: Mheshimiwa Spika, awali ya yote kwanza naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Fakharia kwa jitihada zake kubwa anazochukua katika kukabiliana na changamoto mbalimbali katika Majimbo ya Mkoa mzima wa Mjini. Mimi ni shahidi ni Mbunge ambaye anashirikiana nami vizuri katika Jimbo langu ambalo lipo katika Mkoa wake katika kukabiliana na changamoto hizo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, baada ya pongezi hizo za dhati kwa Mheshimiwa Fakharia naomba sasa nijibu maswali yake kama ifuatavyo:
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa amekiri ameridhishwa na jitihada ambazo tumeshaanza kuchukuwa katika kukarabati uzio kwa upande uliopo karibu na school ya Jang’ombe nimhakikishie kwamba jitihada hizo ambazo zimeanza ndizo ambazo tutaendelea nazo katika kukamilisha uzio wote lakini pamoja na kukarabati nyumba za Askari Polisi pale ambapo fedha zitakapokuwa zimepatikana kama ambavyo nimejibu katika jibu langu la msingi.(Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved