Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Riziki Shahari Mngwali

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. RIZIKI S. MNGWALI aliuliza:- Kwa mila zetu za Kiafrika imezoeleka kuwa huduma ya ukunga kwa akinamama wajawazito wakati wa kujifungua hutolewa na wataalam wanawake:- Je, Serikali haioni kuwa kwa kuweka Wakunga wanaume katika baadhi ya zahanati za Serikali nchini ni kuwadhalilisha akinamama wajawazito wanaojifungua katika zahanati hizo?

Supplementary Question 1

MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba niulize maswali mawili ya nyongeza hasa kwa kuwa majibu hayakutosheleza haja.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunarudi pale pale kwenye kutoa huduma stahiki na kuajiri wahudumu stahiki, siyo suala la kuajiri wengi bali waajiriwe Wakunga ambao wanaendana na mila na desturi zetu na wale ambao wanakidhi haja. Je, Mheshimiwa Waziri atakubaliana na mimi kwamba Serikali hii ya CCM imekuwa inafanya mambo yake kanyaga twende tu na siyo kwa kufuata taratibu maalum?
Mheshimiwa Naibu Spika, je, Serikali hii ya CCM itakubaliana na mimi nikisema kwamba haiendani na matamko yake? Leo hii gazeti linaandika kuboresha huduma za uzazi lakini wanatuambia wataendelea kutuwekea Wakunga wanaume kwa kuwahudumia wanawake. Naomba majibu.

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza Serikali ya Chama cha Mapinduzi haifanyi mambo yake ya kanyaga twende. Hapa nilizungumzia sheria inasemaje kwa sababu kama Majaji Naibu Spika mna taratibu na sheria zenu. Nimeshangaa sana, kuna sehemu nyingine sasa hivi hata ukiangalia kuna ma-gyno wengi sana akinamama lakini siku nyingine wanaenda kwa ma-gyno wa pande zote mbili. Niseme kwamba siku zote Serikali inalenga kuona ni jinsi gani itawasaidia wanajamii kupata huduma bora.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kuhusiana na dhana nzima ya kusema kwamba tuwe tunaajiri watumishi wa kike na wa kiume, nimesema kwamba tutaendelea kuajiri na ndiyo maana nimesema jamii zetu zinatofautiana. Kuna maeneo mengine ambayo inaonekana kwa mila na desturi zao itabidi tuweke watu wa aina fulani na sisi tutafanya hivyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge katika Mkutano uliopita aliuliza swali hili hili na nilitoa maelekezo. Bahati nzuri hapa tumepata takwimu wataalam wangu wa afya na RMO wetu wa Mkoa baada ya agizo lile waliweza kufanya mchakato katika kila zahanati takribani nane wameweza kubadilisha wale wataalam kutokana na swali lako mama la msingi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimepata taarifa hizo lakini nitaenda kufanya verification mwenyewe kuona hali ikoje, lakini taarifa nilizozipata toka wiki iliyopita ni kwamba walifanya mchakato huo na zile zahanati ambazo mwanzo zilikuwa na wataalam wa kiume peke yake sasa hivi wamepeleka na wataalam wa kike lengo likiwa ni kuwasaidia akinamama.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwa Wilaya ya Mafia, napenda kuwashukuru sana kwa mchakato mlioufanya wa kupata mashine mbalimbali. Tulikuwa na tatizo la X-ray na Utra-sound machine, Mbunge wao Mheshimiwa Dau amefanya harakati watapata Ultra-sound na X-ray machine mpya, zimeshafika Dar es Salaam sasa hivi wanaendelea na taratibu za kuzisafirisha kwenda Mafia. Kwa hiyo, tutaendelea kuenzi juhudi kubwa zinazofanyika lakini Serikali itajitahidi kwa kadiri iwezekanavyo wananchi wapate huduma bora.