Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Primary Question

MHE. ALEXANDER P. MNYETI Aliuliza: - Chanzo cha Maji cha Ihelele kilichopo Kijiji cha Nyanhomango kinasambaza maji katika Mikoa ya Shinyanga na Tabora: - Je, ni lini Serikali itapeleka miundombinu ya maji kwenye Kijiji hicho pamoja na vijiji vingine vinavyozunguka chanzo hicho?

Supplementary Question 1

MHE. ALEXANDER P. MNYETI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi hii. Nianze kwa kusikitika sana kwamba majibu anayoandaliwa Mheshimiwa Naibu Waziri na wataalam mengi ni ya uongo. Anaposema kwamba kule Nyanhomango maji yapo milioni ngapi sijui, ni uongo mtupu.

Mheshimiwa Spika, nataka nikwambie mimi ile Ihelele tunayoisema ndiyo chanzo kikubwa cha maji kinachopeleka maji Tabora, Nzega, Kahama, Shinyanga na maeneo mengine. Sisi hatuna tatizo na maji yanakwenda wapi; sisi shida yetu ni tupate maji kwenye kijiji hicho na maeneo yanayozunguka. Ni chanzo kikubwa lakini leo ni zaidi ya miaka 15 wananchi bado wanahangaika na maji kwenye eneo hilo.

Mheshimiwa Spika, sasa kinachosikitisha ni hao wataalam wetu walioko huko. Mimi nimemaliza ziara juzi pale; hakuna hata tone la maji. Hizo DP anazozisema Mheshimiwa Naibu Waziri ni kwamba ma-DP yamewekwa zaidi ya miaka 10 yanakwenda Mbarika halafu hayatoi hata maji. Sasa majibu haya Wanamisungwi wajue tu kama hamtaki kupeleka maji, lakini majibu haya yametolewa miaka 15 iliyopita yanaendelea kutolewa hayohayo, hatuwezi kufurahishana kwa staili hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hawa wataalam wanaoandaa haya majibu kwenda kwa Naibu Waziri, ni majibu ya uongo na wanatakiwa kuchungwa.

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kwanza nikushukuru sana na nimpongeze Mheshimiwa Mbunge lakini nataka nimhakikishie kwamba Serikali inafanya jitihada kubwa sana katika Jimbo lake la Misungwi. Hivi karibuni tulikuwa na Mheshimiwa Rais na tumezindua mradi wa bilioni 12 katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, maji hayana mbadala na sehemu kwenye chanzo toshelezi, maelekezo ambayo tumeyatoa sisi kama Wizara ya Maji ni kuhakikisha kwamba kabla hatujapeleka maji maeneo mengine, wananchi wa maeneo husika lazima wapate huduma ya maji.

Kwa hiyo, ninachotaka kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge, nimuombe saa saba tukutane na mimi niko tayari kuongozana naye kufanya ziara ili kwenda kujionea uhalisia na kuweza kutoa msaada katika eneo lile ili wananchi waweze kupata huduma ya maji. Ahsante sana. (Makofi)