Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Omari Mohamed Kigua
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilindi
Primary Question
MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza:- Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Serikali itaanza mkakati wa kusambaza maji kutoka Mto Dibuluma kata ya Kibati Wilaya ya Mvomero na kuyasambaza katika kata ya Tunguli, Kwekivu, Masagalu na Songe Wilayani Kilindi?
Supplementary Question 1
MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri na Waziri wake wa maji kwa kututengea kiasi cha shilingi bilioni 2,146,000,000 kwa ajili ya huduma kwa watu wa Kilindi, baada ya shukrani hiyo ningependa tu nimuulize swali moja tu Mheshimiwa Naibu Waziri.
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na maelezo mazuri ya kwamba wanafanya tafiti na tafiti hiyo itatoa majibu ndani ya mwezi ujao, sasa nataka tu kupata commitment ya Mheshimiwa Naibu Waziri je, wananchi wa Wilaya ya Kilindi wategemee nini kuhusiana na uhakika wa mradi wa huu ambao utahudumia zaidi ya vijiji 12? Ahsante. (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Omari Mohamed Kigua kama ifautavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nipende kupokea pongezi zake kwangu pamoja na Mheshimiwa Waziri kwa hakika tunashirikiana vema na wewe pia nikupongeze kwa sababu unatupa ushirikiano mzuri na tutaendelea kufanya kazi bega kwa bega kuhakikisha suala la maji tunakwenda kulitatua kwa pamoja.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na lini sasa commitment ya serikali kwenye Mradi huu wa Diburuma ni kwamba tayari kama nilivyoeleza kwenye jibu langu la msingi utafiti unaendelea na hivi punde mwezi ujao tunakwenda kukamilisha usanifu hivyo kutokana na gharama ambayo itapatikana sisi kama Serikali tumejipanga kuhakikisha kutumia chanzo hiki tukiamini kabisa kitakuwa ni chanzo endelevu na sehemu kubwa zaidi ya vijiji 10 ninafahamu zitapitiwa kwa hiyo tutaendelea kushirikiana kuona kwamba chanzo hiki tunakwenda kukitumia tutakitafutia fedha ili kuona kwamba tunatimiza azma ya kuleta maji.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved