Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA aliuliza:- Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ni sehemu ya ghala la chakula la Taifa katika mikoa mitano (5) inayolima chakula kwa wingi nchini Tanzania; lakini kikwazo kikubwa ni usafirishaji wa mazao kufikia masoko ya nje ya Wilaya; Halmashauri imeomba ongezeko la bajeti ya barabara kufikia shilingi bilioni 7,969,000 ili kuweza kukarabati barabara zote muhimu na kuwezesha wakulima kusafirisha mazao yao kwa urahisi na hatimaye kuongeza kipato cha Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe:- Je, Serikali ipo tayari kukubali ombi la Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe la kuongeza fedha katika bajeti ya 2016/2017?

Supplementary Question 1

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Ahsante. Kwa kuwa Waziri amekiri kwamba bajeti iliyopita walitenga milioni 870, lakini ni milioni 157 tu ndiyo zimepelekwa. Je, haoni umuhimu wa kuhakikisha pesa iliyobaki inapelekwa.
Swali la pili, kwa kuwa Halmashauri ya Rungwe imepata mafuriko na uharibifu wa barabara umekuwa mkubwa sana, naomba Wizara hii itutumie pesa za haraka kwa ajili ya emergency kwa ajili ya vijiji kama tisa zaidi ya kilometa 40; kama Kijiji cha Kyobo, Ikuti na sehemu za Lupepo. Je, Serikali haioni umuhimu wa kupeleka pesa hizo haraka kwa ajili ya kusaidia barabara na madaraja yaliyoharibika?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli katika majibu yangu ya msingi nilisema bajeti ilikuwa ya shilingi milioni 870, zilizopelekwa mpaka sasa ni shilingi milioni 157, jibu hili nimekuwa nikilitoa kila mahali katika vipindi mbalimbali. Nilisema wazi, ukiachia changamoto ya ujenzi wa barabara, lakini kuna miradi mingi kipindi kilichopita ilikuwa haiendi vizuri. Nilitolea mifano miradi ya maji na miradi mingineyo kwamba upelekaji wa pesa ulikuwa ni tatizo kubwa sana, lakini kulikuwa na sababu zake za msingi. Katika mwaka uliopita pesa nyingi sana zilienda katika matukio makubwa ambayo yalikuwa yamejitokeza kama suala la uandikishaji na uchaguzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mchakato wa hivi sasa, Serikali imejielekeza zaidi katika ukusanyaji wa mapato, ndiyo maana hivi sasa hata ukiangalia kwa mara ya kwanza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imevunja rekodi katika ukusanyaji wake wa mapato. Nilisema kwamba hata miradi iliyokuwepo mwanzo imesimama, lakini hivi karibuni miradi hiyo inapelekewa fedha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nia yetu ni kwamba, katika kipindi hiki cha bajeti kilichobakia nina imani Serikali itajitahidi kupeleka fedha katika miradi yote iliyosimama nikijua wazi katika maeneo hayo mengine wakandarasi ambao ni wa ndani na wengine wa nje wanaendelea kudai. Kwa hiyo, suala hili tunaweka kipaumbele siyo kwa ajili ya maeneo hayo tu isipokuwa kwa Tanzania nzima kwa ujumla.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mafuriko na kuharibu miundombinu ya barabara, hili nilisema ni kweli. mwaka huu ukiangalia maeneo mbalimbali tumekuwa na changamoto ya mvua kubwa iliyonyesha. Nimetolea mfano kule Rungwe, ukienda Kyela, ukienda Kilosa na maeneo mbalimbali, yote yameathirika kwa ajili ya mvua na ndiyo maana tulipeleka utaratibu kwamba kila Halmashauri ianishe uharibifu wa miundombinu mara baada ya mvua ile kunyesha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jukumu letu kubwa ni kuangalia sasa kile ambacho tunaweza kusaidia kwa kipindi cha sasa. Kwa hiyo, baada ya uharibifu huo, Serikali itachukua jukumu la kusaidia siyo maeneo ya Rungwe peke yake, isipokuwa maeneo mbalimbali ambayo yameathirika na nafahamu hata maeneo ya Morogoro hali ilikuwa mbaya sana na maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Name

Dr. Charles John Tizeba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buchosa

Primary Question

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA aliuliza:- Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ni sehemu ya ghala la chakula la Taifa katika mikoa mitano (5) inayolima chakula kwa wingi nchini Tanzania; lakini kikwazo kikubwa ni usafirishaji wa mazao kufikia masoko ya nje ya Wilaya; Halmashauri imeomba ongezeko la bajeti ya barabara kufikia shilingi bilioni 7,969,000 ili kuweza kukarabati barabara zote muhimu na kuwezesha wakulima kusafirisha mazao yao kwa urahisi na hatimaye kuongeza kipato cha Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe:- Je, Serikali ipo tayari kukubali ombi la Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe la kuongeza fedha katika bajeti ya 2016/2017?

Supplementary Question 2

MHE. CHARLES J. TIZEBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kuniona. Kwa kweli, pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri ningependa tu kujua baada ya Halmashauri zetu kuleta haya maombi na ilikuwa katika matarajio yetu kwamba uharibifu huu usikutane na msimu mwingine wa mvua kwa sababu uharibifu utakuwa mkubwa zaidi na bajeti tuliyoipitisha inaweza ishindwe kukidhi hayo mahitaji. Sasa, labda ni lini tu Mheshimiwa Waziri watatuona kabla mvua hazijaanza tena hasa sisi tunaotoka kwenye maeneo ya misimu miwili ya mvua?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini naomba niseme kwamba hapa siwezi kusema kesho au keshokutwa, kwa sababu tunachofanya ni needs assessment. Tuna Halmashauri zipatazo 181, kila Halmashauri ina changamoto yake ya jinsi gani miundombinu ya barabara imeharibika. Kwa hiyo, wataalam wetu wanalifanyia assessment katika maeneo mbalimbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikopita maeneo mengine ni kweli huo uharibifu umekuwa wa kiwango kikubwa sana. Hivi sasa wananchi wengine wanashindwa hata kufika katika maeneo mbalimbali. Kwa hiyo, jukumu letu kubwa ni ku-fast truck hii process ili angalau kitakachopatikana kidogo tuweze kugawana ili wananchi waweze kupata huduma kwa kipindi hiki cha sasa.