Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza: - Je, kuna mkakati gani wa kupata mkopo wa fedha wa muda mrefu kwa masharti nafuu ili kulipa madeni sumbufu ya awamu zote sita?
Supplementary Question 1
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, ahsante pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba niulize maswali mawili ya nyongeza.
Swali la kwanza; kama inavyoonesha, kwamba kila mwaka na kila muda tunalipa Deni la Taifa ni kwa nini sasa Deni la Taifa halioneshi dalili ya kupungua ilhali kila mwaka tunalipa?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, ni lini sasa Serikali italeta mchanganuo wa madeni yote tunayodaiwa kama nchi ili Wabunge tupate fursa ya kushauri katika ulipaji wa madeni hayo? Ahsante.
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Boniphace Mwita Getere, Mbunge wa Bunda kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya kimkakati iliyo mikubwa nchini kwetu. Tunarejesha fedha lakini tuna uhitaji mkubwa tunaendelea kukopa.
Mheshimiwa Spika, kwa swali lake la pili, Serikali inawasilisha taarifa ya madeni yake kwenye Kamati ya Bajeti kila mwaka na kila inapohitajika. Tunaishukuru sana Kamati ya Bajeti kwa miongozo yake inayotusaidia kuendelea kufanya deni letu kuwa himilivu, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved